Featured Kitaifa

WAZIRI NDAKI AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI YA BODI YA NYAMA NCHINI

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi  Mashimba Ndaki,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini uliofanyika jijini Dodoma.

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi  Mashimba Ndaki,akifafanua jambo kwa washiriki wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini uliofanyika jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulia Sekta ya Mifugo Bw.Tixon Nzunda,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini uliofanyika jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Bw.Clemence Tesha,akitoa shukrani baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini uliofanyika jijini Dodoma.

Msajili wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Dkt.Daniel Mushi,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini uliofanyika jijini Dodoma.

WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mashimba Ndaki (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini uliofanyika jijini Dodoma.

…………………………………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi  Mashimba Ndaki,amezindua Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini huku akiitaka kusimamia  soko la nyama ndani na nje ya nchi.

Waziri Ndaki ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizindua  Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Nyama nchini.

Waziri Ndaki amewataka kwenda kusimamia soko la nyama ndani na nje ya nchi ili kuwezesha ukuaji wa soko la nyama pamoja kuongeza mauzo.

” Mauzo ya nyama nje ya nchi yaongezeke Uarabuni wameonesha nia ya kuchukua nyama nyingi kutoka kwetu hivyo nawaomba mkasimamie vyema,”amesema Waziri Ndaki
Aidha amesema kuwa bodi hiyo tayari imeashaanza kupokea wawekezaji na Wafanyabiashara  kutoka nje ya nchi.
“Tukipata wawekezaji wanaopeleka mazao yanayochakatwa nje ya nchi tutaongeza ajira, ni muhimu kutengeza mazingira mazuri yatakayovutia uwekezaji  wa ndani na nje ya nchi,” amesisitiza.
Amesema kuwa Wizara imejipanga kusimamia na kufuatilia kwa umakini utendaji wa Taasisi zote zilizo chini ya sekta ya mifugo Iii kuhakikisha zinajiendesha vizuri, si kwa hasara bali kwa faida .
Waziri Ndaki amesema kuwa Bodi hiyo inategemewa sana katika kusimamia na kukuza soko la nyama ndani na nje ya nchi.
Mhe Ndaki amesema kuwa Bodi hiyo ni ya nne’ tangu kuundwa kwa Bodi ya Nyama Tanzania mwaka 2008 .
“Utendaji kazi wenu ukaongozwe na sheria,kanuni  na taratibu,na kuzingatia sheria ya tasnia ya nyama namba 10 ya mwaka 2006 ,kanuni zake sita pomoja na sheria nyingine za nchi, kwa kufanya hivyo mtaweza kutekeleza kazi zenu kwa weledi na ufanisi mkubwa,” ameeleza.
Aidha ameitaka  Bodi hiyo kuandaa mpango wa mabadiliko wa bodi, kusimamia mipango mikakati mizuri ya kuongeza huduma za biashara ya nyama hapa Nchini kwa kutumia vizuri fursa zilizoibuka, kusimamia na kutatua migogoro mahali pa Kazi  inayosabanishwa na migongamo ya kimaslahi na ukiukwaji wa maadili ya Utumishi wa umma ili kuwa na raslimali watu yenye kuleta tija na ufanisi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Nyama Tanzania Clemence Tesha,amesema kuwa watafanya kazi kwa weledi na ufanisi kwa kufuata maagizo yaliyotolewa.

‘Tunakupongeza Mhe Waziri kwa kutuamini tunakuahidi tutafanya kazi kwa weledi kwa kufuata Sheria,taratibu na kanuni ili tuweze kusimamia vyema mapato’amesema Bw.Tesha

About the author

mzalendoeditor