Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI ORKESUMET

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Orkesumet uliopo Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara leo tarehe 15 Machi 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea maelezo ya eneo la mtambo wa kusafisha maji uliopo Loiborsoit Wilaya ya Simanjiro mkoani manyara  kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga wakati alipotembelea na kukagua mradi hu oleo tarahe 15 Machi 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi wa eneo la Loiborsoit mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Orkesumet uliopo Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara leo tarehe 15 Machi 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akicheza wimbo wa kabila la wamaasai wakati alipofika katika eneo la Loiborsoit kuweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Orkesumet uliopo Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara leo tarehe 15 Machi 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwasili na kukagua eneo la chanzo cha maji cha Eltibu kinachotumika katika mradi mkubwa wa maji wa Orkesumet uliopo Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara leo tarehe 15 Machi 2022.

About the author

mzalendoeditor