Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA KISWAHILI

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na washiriki wa  Kongamano la Pili la Idhaa za Kiswahili Duniani, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo  uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC) leo tarehe 14 Machi 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizindua kitabu cha Matumizi ya TEHAMA katika Tasnia ya Habari kilichoandikwa na Victor Elia, Mtumishi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Idhaa za Kiswahili Duniani, uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea tuzo ya Nishani ya Heshima ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mtumiaji mahiri wa lugha ya Kiswahili aliokabidhiwa na Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Idhaa za Kiswahili Duniani, uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea tuzo ya Nishani ya Heshima ya kuwa mtumiaji mahiri wa lugha ya Kiswahili aliokabidhiwa na Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Idhaa za Kiswahili Duniani, uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizindua Kamusi Kuu ya Kiswahili Toleo la 3 wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Idhaa za Kiswahili Duniani, uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC) 

………………………………………………

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 14 Machi 2022 amefungua Kongamano la Pili la Idhaa za Kiswahili Duniani, ufunguzi uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha (AICC).

Makamu wa Rais amewaasa wataalamu, mabingwa na wapenzi wa lugha ya Kiswahili kuendelea kuandika vitabu vya taaluma mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili ili kuepusha ongezeko la upotoshaji wa matumizi  wa lugha ya Kiswahili miongoni mwa jamii husasani  wanahabari  wanaotumia maneno yasiyo rasmi au kuchanganya kiswahili na maneno ya lugha nyingine.

Amesema ubunifu unahitajika  katika ufundishaji na uwasilishaji wa lugha ya Kiswahili kwa kutumia teknolojia ya kisasa, ili kuendana na kasi ya maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Aidha amesema Katika tasnia ya habari, ni muhimu kuwa na vifaa bora vitakavyowezesha maarifa ya lugha hii yafike popote yanapohitajika kwa haraka na ufasaha. 

Makamu wa Rais ameongeza kwamba  Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ipo tayari kushirikiana na Taasisi na wadau mbalimbali katika kusimamia kwa karibu Mkakati wa Taifa wa kubidhaisha Kiswahili ambao utazinduliwa rasmi siku ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani na kuhakikisha kuwa unatekelezwa kikamilifu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Amesema Serikali itaendelea kuhamasisha ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni kupitia Balozi na kujenga ushawishi kwa nchi nyingine kuingiza Kiswahili katika mitaala ili kuendelea kusambaza lugha hiyo.

Awali akimkaribisha Makamu wa Rais, Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amesema wizara itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wataalamu wa lugha ya kiswahili ili waweze kutumia fursa mbalimbali za lugha hiyo kama vile ukalimani, tafsiri, ufundishaji, uhariri na uandishi wa vitabu na majarida. Ameongeza kwamba wizara imeandaa kanzi data ili kuwatambua wataalamu wa kiswahili nchini katika ngazi zote.

Kwa upande wake kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) Consolata Mushi amesema Kongamano hilo litasaidia kubadilishana uzoefu na kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowapata wanahabari katika kutumia Kiswahili katika kazi zao. Amesema uzinduzi wa  Kamusi Kuu ya Kiswahili Toleo la 3 utaongeza ufanisi katika tasnia ya habari kwa idhaa zinazotumia lugha ya Kiswahili kutokana na uwepo wa maneno zaidi ya mia moja mapya.

Kongamano hilo la siku tano linabeba kauli mbiu isemayo Tasnia ya Habari kwa Maendeleo ya Kiswahili Duniani huku likishirikisha wadau wa Kiswahili na vyombo vya habari kutoka ndani na nje ya nchi.

About the author

mzalendoeditor