Featured Michezo

WAZIRI MCHENGERWA AIAGIZA TFF KUONGEZA VIWANJA VIWILI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameliagiza Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania TTF kuongeza viwanja viwili kimoja cha nyasi bandia na kingine cha nyasi za kawaida ili idadi ya viwanja vinavyojengwa katika mradi wa ujenzi wa kituo cha michezo Tanga ifikie vinne.

Mhe. Mchengerwa ametoa agizo hilo leo Machi 13, 2022 baada ya kufanya ziara kuangalia mwenendo wa ujenzi wa kituo cha michezo cha Tanga kinachojengwa katika eneo la Mnyanjani kwa ufadhili wa Fifa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema kutokana na kiu ya watanzania kutumia miundombinu yenye sifa, na uwepo wa eneo kubwa linalotosha kujengwa kwa viwanja mbalimbali, TFF wanapaswa kuongeza viwanja viwili kama hatua ya kujidhatiti katika kumaliza changamoto ya miundombinu hafifu ya michezo na hasa viwanja kwa upande wa soka.

Pamoja na kuagiza kujengwa kwa viwanja hivyo viwili pia Waziri Mchengerwa ameagiza TFF kujenga uzio kuzunguka eneo hilo haraka iwezekanavyo kama hatua ya kuweka usalama wa rasilamali zilizopo uwanjani hapo na kupunguza mwingiliano baina ya jamii na shughuli za TFF.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) Wallace Karia, amesema wamepokea maelekezo ya Waziri Mchenegerwa na watayafanyia kazi haraka iwezekanavyo na kushauli uungwaji mkono na serikali katika kujenga majengo miundo mbinu yenye mfano na hiyo katika maeneo mbalimbali ili kuongeza wigo.

Katika mahojiano na waandishi wa habari mwenyekiti wa soka la vijana Tanzania Khalidi Abdalah Mohamed, amesema uwepo wa kituo hicho katika kanda ya kasikazini kitakachogharimu kiasi cha dola milioni mbili na elfu 44 ni jambo la faraja katika kukuza vipaji vya vijana.

About the author

mzalendoeditor