Featured Michezo

RONALDO AVUNJA REKODI YA MABAO YA FIFA,MAN UNITED IKIICHAPA SPURS

Written by mzalendoeditor

MSHAMBULIAJI wa Manchester Uniteda na Timu ya Taifa ya Ureno  Cristiano Ronaldo  amevunja rekodi ya mabao ya FIFA baada ya kufunga hat-trick na kuiwezesha Man United kuizamisha mabao 3-1 dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford. 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 sasa amefikisha mabao 807, akimpiku Josef Bican, aliyekuwa anashikilia rekodi hiyo.
Ronaldo alifunga mabao yake dakika za 12, 38 na 81, wakati mabao ya Spurs yalifungwa na Harry Kane kwa penalti dakika ya 35 na Harry Maguire aliyejifunga dakika ya 72.
Kwa ushindi huo  Man United ifikishe pointi 50 katika mchezo wa 29 na kurejea nafasi ya nne, ikiizidi pointi mbili Arsenal, ambayo hata hivyo ina mechi nne mkononi, wakati Spurs inabaki na pointi zake 45 za mechi 27 sasa nafasi ya saba.

About the author

mzalendoeditor