Featured Kitaifa

RAIS DK.MWINYI AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA UWEKEZAJI SEKTA YA MAJI BARANI AFRIKA

Written by mzalendoeditor

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua Mkutano Mkuu wa Uwekezaji wa Sekta ya Maji Barabi Afrika uliofanyika Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Melia Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 11-3-2022. Uliowashirikisha wadau mbalimbali. Tanzania na Nje ya Tanzania (Picha na Ikulu).

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akionesha Kitabu cha Mpango wa Miaka Mitano ya Uwekezaji katika Sekta ya Maji Zanzibar, baada ya kuzindua mpango huo, wakati ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Uwekezaji wa Sekta ya Maji Barani Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Melia Kiwengwa na (kulia kwa Rais) Rais Mstaafu wa Tanzania Mwenyekiti wa Taasisi ya (GWPSA) Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Maji,Nishati na Madini Zanzibar Mhe.Shaib Hassan Kaduara.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na (kulia kwa Rais) Rais Mstaafu wa Tanzania Mwenyekiti wa Taasisi ya (GWPSA) Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Maji,Nishati na Madini Zanzibar Mhe. Shaib Hassan Kaduara, wakifuatilia Mada ikiwasilishwa wakati wa mkutano huo Mkuu wa Uwekezaji wa Sekta ya Maji Barani Afrika uliofanyika Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Melia Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 11-3-2022.(Picha na Ikulu)

About the author

mzalendoeditor