Mtu wa kwanza aliyepandikizwa moyo wa nguruwe afariki dunia.
David Bennett, aliyekuwa anaugua ugonjwa sugu wa moyo aliishi kwa miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Marekani.
Hali yake ya kiafya ilianza kudorora siku kadhaa zilizopita. Daktari wake huko Baltimore alisema mwanamume huyo alifariki dunia hapo jana.