Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za mitaa (TALGWU) Mkoa wa Dodoma Siwajibu Peter akikabidhi boksi la taulo za kike kwa Mkuu wa Gereza la wanawake Isanga, Mrakibu Chausiku Kizigo walipotembelea Leo 7,2022 ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
……………………………………………………..
Na Mwandishi wetu-DODOMA
Wafungwa wa Gereza la Isanga wameiomba jamii kuwa na tabia ya kutembelea na kutoa misaada ya kibinaadamu kwa ajili ya kuendesha maisha yao wakiwa gerezani.
Hayo yameyasemwa leo Februari 7, 2022 na baadhi ya wafungwa walipotembelewa na wanawake wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali za mitaa (TALGWU) ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Akizungumza kwa niaba ya wafungwa wengine Edson Mwombeki amesema kutokana na maisha ya kutengana na familia zao, kumewafanya kuwa wapweke na watu wenye uhitaji wa kusaidiwa na kufarijiwa zaidi.
Alisema kutokana na wafungwa wengine kukosa ndugu wanalazimika kushirikiana nao kwenye matumizi ya bidhaa kama sabuni, dawa za meno, mafuta na bidhaa nyingine kwa ajili ya kuendesha maisha yao wakiwa gerezani.
“Humu kuna wafungwa mpaka raia wa kigeni, sasa ukisema usubiri ndugu zao, utawapata wapi? Tunalazimika kutumia vitu ambavyo tunaletewa na ndugu zetu kama sehemu ya kuwasaidia lakini havitoshi”alisema
Naye Mrakibu wa Magereza na Mkuu wa gereza la wanawake Isanga Chausiku Kizigo alikiomba chama hicho na jamii kuwa na desturi ya kutembelea gereza hilo mara kwa mara huku akisema changamoto ni Cherehani ya kushonea nguo za wafungwa zinazochanika.
“Kuna wakati wafungwa nguo zao zinachanika sasa kukiwa na Cherehani wanashona wenyewe tu kwakuwa wengine wana ujuzi lakini pia wafungwa wanahitaji zaidi faraja na kutiwa moyo ili kuendesha maisha yao wakiwa gerezani”alisema
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali za mitaa (TALGWU) mkoa wa Dodoma Siwajibu Peter aliwataka wafungwa hao kuwa wachamungu na kujifunza tabia njema ili wakafute makossa na tasiwra ya uhalifu waliyoiacha kwenye jamii.
Bidhaa walizokabidhiwa kwenye hafla hiyo ni miswaki, viatu, mafuta, taulo za kike, nguo, tishu za chooni, dawa za meno na kulipiwa vifushi vya visumbuzi wanavyotumia.
Previous articleTGNP YASHIRIKI KONGAMANO LA KITAIFA LA WANAWAKE JIJINI ARUSHA
Next articleRAIS SAMIA:TUNATAMBUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM NCHINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here