WENYEJI katika Mchezo wa Soweto Derby Timu ya Orlando Pirates imeshindwa kutamba kwenye  uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Kaizer Pirates mchezo wa Ligi ya Afrika Kusini uliopigwa katika uwanja wa Orlando.

Kaizer walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Reeve Frosler dakika ya 18 bao lililodumu mpaka mapumziko kwa wageni kwenda wakiwa kifua mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote mbili kufanya mabadiliko mnamo dakika ya 81 Kaizer walifunga bao la pili likifungwa na Eric Mathoh huku bao la kufutia machozi kwa Orlando limefungwa na Kwame Peprah dakika ya 55.

Kwa ushindi huo Kaizer Chiefs wamepanda hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 35 wakiwa wamecheza mechi 19 huku Orlando Pirates wakibaki nafasi ya nne wakiwa na Pointi 32 wakiwa wamecheza mechi 22 na Mamelodi Sundowns FC bado wanaongoza msimamo huo wakiwa na Pointi 51 kwa kucheza mechi 22.

VIKOISI:Pirates: 40. Mpontshane, 5. Nyauza, 49. Ndah, 26. Shandu, 29. Mako, 16. Monare, 6. Motshwari, 18. Dlamini, 3. Lorch, 11. Hotto, 46. Peprah

Subs: 31. Ofori, 42. Mabaso, 27. Dzvukamanja, 32. Mntambo, 25. Lepasa, 23. Maela, 17. Jooste, 9. Mabasa, 4. Jele

Chiefs: 1. Petersen, 3. Mathoho, 4. Cardoso, 27. Njabulo Ngcobo, 39. Frosler, 45. Blom, 21. Manyama, 24. Nange, 25. Parker, 10. Dolly, 11. Billiat.

Subs: 43. Bvuma, 2. Mphahlele, 8. Castro, 5. Baccus, 29. Dube, 12. Nkosingiphile Ngcobo, 26. Mabiliso, 14. Sekgota, 33. Radebe.

Previous articleSPIKA DKT. TULIA MGENI RASMI SIKU YA UWEZESHAJI WAJASIRIAMALI WANAWAKE JIJINI MBEYA
Next article‘MARUFUKU UTOAJI WA MIGUU BANDIA KWA WALEMAVU BILA KUWAPIMA’-WAZIRI UMMY

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here