Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akikagua daraja la Tembela na Mwasanga zilizopo katika kata hiyo wakati wa ziara ya kikazi kuhusu mafanikio na mipango ya Serikali katika jimbo hilo leo Machi 4, 2022
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akizungumza na wananchi wa kata ya Tembela na Mwasanga wakati wa ziara ya kikazi kuhusu mafanikio na mipango ya Serikali katika jimbo hilo leo Machi 4, 2022
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Rashid Chuachua na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakati alipofanya ziara ya kikazi kuhusu mafanikio na mipango ya Serikali katika kata ya Tembela ma Mwasanga zilizopo Jimbo la Mbeya Mjini leo Machi 4, 2022
Wananchi wa kata ya Tembela na Mwasanga wakimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza wakati wa ziara ya kikazi katika kata hiyo kuhusu mafanikio na mipango ya Serikali katika jimbo hilo leo Machi 4, 2022
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
…………………………………………..
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshangazwa na Uongozi wa TARURA Mkoa wa Mbeya kuchelewa kuanza ujenzi wa daraja la Tembela-Mwasanga licha ya Serikali kutoa kiasi cha Shilingi billion 1.4.
Akiwa katika ziara ya kikazi leo Machi 4, 2022, Spika Dkt. Tulia amesema kuwa daraja hilo ambalo ni kiunganishi cha kata za Tembela, Mwasanga na Mwakibete kuelekea Mbeya Vijijini liliharibika tangu mwaka 2019 baada ya kusombwa na mafuriko ya mvua na kusababisha maafa kwa wananchi ikiwemo vifo vya watu watano
Dkt. Tulia amehoji ni kwanini Meneja wa Mkoa huo ameshindwa kutekeleza maelekezo aliyopewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa aliyoyatoa Februari 15, 2022 wakati akikabidhi fedha na kuelekeza kwamba ujenzi wa daraja hilo unapaswa kuanza rasmi Machi 1, 2022 na badala yake hakuna hatua iliyofanyika hadi sasa.
“Nilitaraji baada ya Waziri kutoa yale maelekezo basi leo nitakapopita katika daraja lile nitamkuta mkandarasi yupo site anaendelea na ujenzi lakini imekuwa tofauti hakuna kinachoendelea pale, nachotaka kusema hapa ni kwamba tumeshachoka kusubiri kwa miaka yote na tunachohitaji hapa ni kuona daraja na sio vinginevyo” amesema Dkt. Tulia
Akijibu hoja hiyo, Meneja wa TARURA Mkoa wa Mbeya Mhandisi Charles Mwita, amesema kuwa kilichosababisha kuchelewa kwa ujenzi huo ni mchakato wa manunuzi pamoja na kumpata mkandarasi hivyo ameahidi ya kwamba hadi kufikia machi 15, 2022 ujenzi utakuwa umeanza rasmi.