Na Alex Sonna-DODOMA
MABIGWA watetezi Simba SC wameendelea kuifukuzia Yanga kimya kimya baada ya kupata ushindi wa kibabe wa mabao 3-0 dhidi ya Biashara United kutoka Mara Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Bara mchezo uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa.
Simba walipata bao dakika ya 8 kupitia kwa Pape Sakho aliyepokea pasi kutoka kwa Shomari Kapombe na kupiga kiki kali akiwa nje ya boksi la 18 la Biashara na kuzama moja kwa moja nyavuni ilikimshinda kipa James Ssetuba.
Kiungo Mkabaji Mzamiru Yassin aliwainua mashabiki wake baada ya kufunga bao la pili dakika ya 13 akiunganisha kwa kichwa mpira wa krosi uliopigwa na Kapombe.
Mnamo dakika ya 90 Simba walipata tuta baada ya Morrison kuangushwa ndani ya 18 na Meddie Kagere alikosa tuta hilo baada ya kipa James Ssetuba kiindaka hadi mwamuzi wa kati Martin Sanya kutoka Morogoro anapuliza Kipyenga cha mwisho Simba wameibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 34 nafasi ya pili wakizidiwa Pointi 8 na Yanga wenye Pointi 42 huku Biashara United wakibaki nafasi ya 14 kwa Pointi 15.
Mchezo mwingine umechezwa uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba wenyeji Kagera Sugar wameshindwa kutamba katika uwanja wao baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC kutoka Lindi