Featured Kitaifa

MTOTO AMUUA BABA YAKE MZAZI 

Written by mzalendoeditor

Na Lucas Raphael,Tabora 

Jeshi La Polisi Wilayani Nzega mkoani Tabora linamshikilia MICHAEL Jacob(25) kwa tuhuma za kumua Baba yake Mzazi kwa kumkata kwa shoka kichwani, Shingoni na mikono yote miwili kutokana na imani za Kishirikina.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao kwa waandishi wa habari alisema kuwa Tukio hilo limetokea February 28 mwaka huu majira ya saa 1 usiku katika kijiji cha Upungu Tarafa ya Puge Wilaya ya Nzega mkoani hapa

Kamanda Abwao akizungumzia  mauaji hayo ya baba kuuwa na mwanawe wa kiume kwa kutumia Shoka alisema kuwa siku hiyo Mtuhumiwa ambaye anashikiliwa lilifanyika majira ya  saa moja  usiku katika kitongoji na kijiji cha  upungu mashariki.

Kamanda huyo wa polisi alimtaja baba aliyeuawa kuwa ni  Jacob mbela mzee wa miaka (88) na kwamba chanzo cha mauaji hayo ni imani za Kishirikina.

Aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo pia mara baada ya kufanya mauaji hayo ya kinyama pia alijeruhi dada yake aliyetambuliwa kwa jina la Magdalena Jacob ambaye alitibiwa hospitali na kuruhusiwa.

Alisema kuwa mtuhumiwa Michael Jacob ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa alichuku jukumu la kumuua baba yake kutokana na kile alichodai kwamba ugonjwa huo aliupata baada ya kulongwa na baba yake huyo.

Kamanda Abwao alisema kuwa Mtuhumiwa baada ya kufanya mauaji hayo ya kinyama alitoweka eneo la nyumbani na kwenda kujificha lakini  kulifanyika msako mkali ulifanikisha kumkamata akiwa katika kijiji jirani na hapo tukio la mauaji lilipofanyika.

Alisema kwamba kuwa mara  baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo ,alikiri kufanya mauaji ya baba yake kwa shoka ambalo ndilo kielelezo cha kwanza na hatafikishwa mahakamani kujibu Tuhuma za mauaji.

Hata hivyo mtuhumiwa huyo pia alimjeruhi dada yake Magdalena Jacob ambaye alitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani na hali yake inaendelea vizuri  .

About the author

mzalendoeditor