Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA YA MAJIVU NAIROBI

Written by mzalendoeditor

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 2 Machi 2022 akiwa Jijini Nairobi ameshiriki ibada ya Jumatano ya majivu katika kanisa la Mtakatifu Paulo mtaa wa chuo kikuu cha Nairobi.

Akiongoza Ibada hiyo Paroko msadizi wa Kanisa katoliki la Mtakatifu Paulo Padri Edwin Hunja  amewataka waumini kutumia kipindi hiki cha kwaresma katika kutafuta msamaha na huruma ya mwenyezi Mungu pamoja na kujielekeza kutenda matendo yaliyo mema. Padri Paulo amesema mwezi huu wa Kwaresma unapaswa kutumika katika kuwapatanisha wale wanaofarakana na kombea dunia kuwa sehemu ya Amani.

Ibada ya majivu kwa waumini wa Imani ya kikristo ni mwanzo wa mfungo na kipindi cha kwaresma kuelekea sikukuu ya pasaka.

About the author

mzalendoeditor