Featured Kitaifa

KIPANGA ARIDHISHWA NA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA WIZARA YA ELIMU MTUMBA DODOMA

Written by mzalendoeditor

NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akisikiliza taarifa ya mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini  Dodoma ikisomwa na Mkadiliaji majenzi kutoka chuo cha Ardhi Bw.Saudeni Anania,wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo leo March 2,2022 

NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akizungumza mara baada ya kupokea  taarifa ya mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini  Dodoma iliyosomwa na Mkadiliaji majenzi kutoka chuo cha Ardhi Bw.Saudeni Anania,wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo leo March 2,2022 

NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akikagua  mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini  Dodoma wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo leo March 2,2022 

Mafundi ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini  Dodoma wakiendelea na ujenzi huo.

NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akimsikiliza Meneja Mradi kutoka kampuni ya CRJE Bw.Li Yang wakati wa ziara ya kukagua  mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini  Dodoma  leo March 2,2022 .

NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi ya kukagua   mradi wa ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini  Dodoma  leo March 2,2022 .

……………………………………………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omary Kipanga ameridhishwa na ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Mtumba Jijini hapa ambapo amemtaka  Mkandarasi anaetekeleza mradi  huo kutoka kampuni ya CRJE kukamilisha kwa wakati.

Amesema wao kama Wizara watahakikisha wanausimamia mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati.

Akizungumza leo Machi 3,2022 jijini Dodoma mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi hiyo Mtumba Naibu Waziri Kipanga amesema mradi huo unaendelea vizuri na ameridhishwa  na jinsi ambavyo unatekelezwa.

“Nimpongeze sana Mkandarasi kwa kuweka Programu ya kazi pamoja na vitendea kazi vipo vizuri unapofanya kazi kama hii ni lazima uwe na rasilimali watu,rasilimali fedha, material,muda,Menejimenti ndio maana nilihitaji kuona hivi .Tunaamini tukisimamia vizuri kazi yetu itaenda vizuri,”amesema

Amesema  Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia  watahakikisha wanausimamia mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati.

“Sisi Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia tutahakikisha tunasimamia ujenzi huu kwa kushirikiana na wenzetu wa Chuo Kikuu cha Ardhi ambao ndio washauri wa mradi ili kazi hii iweze kukamilika,”amesema.

Amesema mradi huo  umeanza tangu Desemba  15  mwaka  2021 na unatarajiwa kukamilika   Desemba 15 mwaka  2023 ambapo zaidi ya shilingi bilioni 15 zinatarajiwa kutumika na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameishatoa fedha hizo.

“Litakapokuwa limekamilika tunakadiria si chini ya shilingi bilioni 15 ambapo fedha hizo tayari Rais Samia Suluhu Hassan ameishazitoa kwa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.Haya sio kwenye Wizara ya elimu tu yanajengwa katika Wizara na Taasisi zote,”amesema.

Kwa upande wake Mkadiliaji majenzi kutoka chuo cha Ardhi Bw.Saudeni Anania,amesema awamu ya pili ya ujenzi huo inajumuisha ujenzi wa jengo la ofisi lenye jumla yay a sakafu nane,sakafu ya ardhini (basement),chini (Graund Floor na za juu sita (six upper floors) ambapo sakafu ya nane ni ya kukaa mitambo ya huduma wezeshi za jengo.

Amesema pia kuna kazi za nje ambazo ni ujenzi wa maegesho ya magari,bustani pamoja na fensi ambapo amedai jengo hilo linakadiriwa kuwa na jumla ya eneo la sakafu la mita za mraba 10900.

Amesema mradi huo unaendelea vizuri ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 5.

“Rai yetu kwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa pamoja tunaomba juhudi zaidi katika ufuatiliaji wa malipo ya mkandarasi pindi ambapo nyaraka zinapohusu malipo zinapowafikia kutoka kwa mshauri elekezi  ili kuepusha ucheleweshwaji wa mradi,”amesema.

About the author

mzalendoeditor