Featured Kitaifa

KAMATI YA WAZAZI WA WATOTO WANAOSOMA UKRAINE WAKUTANA NA WAZIRI MKENDA NA BALOZI MULAMULA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda akizungumza katija kikao cha pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na kamati ya wazazi wenye watoto wanaosoma Ukraine

Mkurugenzi wa Taasisi ya Global Education Link Abdul Miloel akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Kamatu ya Wazazi wenye watoto wanaosoma Ukraine

…………………………………………………………….

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula leo Machi 2,2022 wamekutana na kamati ya wazazi wenye watoto wanaosoma Ukraine kutoa na kupokea taarifa ya hali ya usalama ya wanafunzi hao.

Akizungumza katika kikao hicho Prof Mkenda ameipongeza Serikali kwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa katika kuhakikisha usalama wa Wanafunzi walioko Ukraine pamoja na hatua za kuwawezesha kurejea.

” niwaombe wazazi mnapoongea na Vijana wetu walioko huko wawe na utulivu na kwamba Serikali yao inafanya jitihada kuhakikisha usalama wao na pia wafuate maelekezo ya kiusalama yanayotolewa na Mamlaka za nchi hiyo”

Kuhusu kuendelea na masomo wanafunzi watakaorejea nchini kuendelea Waziri huyo amesema Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojoa , itakutana na wanafunzi hao na kuona utaratibu utaokafaa kuwawezesha kuendelea na Masomo yao wakiwa nchini.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Global Link Abdul Mollel ambayo ndio iliyoratibu wanafunzi hao kusoma katika Vyuo mbalimbali Nchini Ukraine ameishuruku Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuwa tayari kuona namna ya kuwasaidia Wanafunzi kuendelea na Masomo watakaporejea.

About the author

mzalendoeditor