RAIS huru Kenyatta apongeza uwamuzi wa chama tawala cha Jubilee kumunga mkono mpinzani wake wa zamani Rais Odinga wa chama cha ODM kugombania kiti cha rais.
Chama tawala cha Kenya, Jubilee kimetangaza kumunga mkono Raila Odinga, kiongozi mkongo wa upinzani katika juhudi zake za kugombania kiti cha rais wakati wa uchaguzi mkuu wa Ogusti mwaka huu.
Uwamuzi huo muhimu unamuondoa Naibu Rais Wlliam Ruto kua mgombea wa chama hicho licha ya kwamba ametangaza anagombania kiti cha rais.
Mkutano wa Wajumbe wa Taifa wa chama cha Jubilee, NDC, ulofanyika mjini Nairobi siku ya Jumamosi kilitangaza pia mabadiliko kwenye uwongozi wake, kwa kumuondosha Ruto kama naibu mwenyekiti.
Nafasi ya Ruto inachukuliwa hivi sasa na Jimmy Angwenyi, na katibu mkuu wa chama Raphael Tuju anaondoka na nafasi yake inachukuliwa na Jeremiah Kioni, mbunge wa Ndaragwa.
Odinga mwenye umri wa miaka 77, aligombania nafasi ya kiti cha rais mara nne akiwa mgombea kutoka nje ya serikali, akiahidi kuleta mabadiliko lakini hakufanikiwa kupata ushindi.
Hivi sasa ameungana na aliyekua mpinzani wake Uhuru Kenyatta aliyemunga mkono rasmi wiki hii.
Uwamuzi huo unaweza kufikisha kikomo mvutano na uhasama wa miongo kadhaa kati ya makabila mawili makuu ya Kenya ya wa-Kikuyu na wa-Luo.
Kenyatta ambae hatoweza kugombia kiti cha rais baada ya kukamilisha mihula yake miwili aliamua kumunga mkono Odinga dhidi ya naibu wake Ruto ambae amesema hafai kua rais wa Kenya.