Featured Kimataifa Uncategorized

‘SIWEZI KUWAACHA WANANCHI WANGU WAKATI NCHI IPO GIZANI’-RAIS ZELENSKY

Written by mzalendoeditor
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amekataa ofa ya Marekani ya kumsaidia kuondoka Ukraine ili kuokoa maisha yake wakati majeshi ya Urusi yakiwa yameuzingira mji huo ambapo amenukuliwa akisema; 
“Unapotushambulia, utaona nyuso zetu, siyo migongo yetu”.
Shirika la Habari la Associated Press limeeleza likimnukuu afisa mmoja wa kijasusi kutoka Ikulu ya White House ya Marekani, akieleza kwamba rais huyo amekataa ofa ya kutoroshwa na Marekani na kuahidi kuendelea kuipigania nchi yake mpaka tone lake la mwisho la damu.
Msimamo wa Volodymyr wa kuamua kuingia mwenyewe mstari wa mbele wa vita, umesifiwa na wengi hususan katika mitandao ya kijamii, hasa baada ya kujirekodi kipande cha video na kukanusha habari zilizokuwa zinaenezwa mitandaoni kwamba ameikimbia nchi yake.

About the author

mzalendoeditor