Featured Kitaifa

MVUTANO:HANANG YASEMA RAMANI INAONESHA CHUMVI IPO KWAO NA SIO BABATI.

Written by mzalendoeditor
Na John Walter-Babati
Ushuru wa madini Chumvi Gedawar umeleta mzozo kati ya Halmashauri ya wilaya ya  Babati na Hanang pande zote mbili zikihitaji kunufaika.
Babati wanasema wanastahili kutumia Ziwa hilo la Chumvi kama chanzo kimojawapo cha mapato huku Hanang nao wakidai wao ndo wanapaswa kulitumia Ziwa hilo.
Kwenye baraza la madiwani February 5,2022 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Babati John Noya amesema Chumvi hiyo inachimbwa katika eneo lao na Hanang lakini ushuru unakwenda Hanang.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Babati John Noya anasema eneo hilo la Mgodi wa Chumvi linahofiwa kuwa na Usalama mdogo kutokana na mvutano huk diwani wa kata ya Arri  Sabini anasema watu wanaoshi upande wa wilaya ya Babati wamekuwa wakpata vipigo bila sababu kutoka kwa askari mgambo wa Hanang.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Anna Mbogo anasema shughuli za kuuza na kusafirisha Chumvi hiyo zinafanyika kwenye utawala wa Babati na kwamba wenye wazo la kutaka kuhamisha mipaka katika bonde hilo wanajisumbua.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Babati wamesema ndani ya mwezi mmoja wanahitaji majibu juu ya jambo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema mazungumzo yameshafanyika kati ya pande zote mbili za wilaya hizo na kwamba kinachosubiriwa kwa sasa ni maamuzi.
Swali ni kwamba yupi anapaswa kuwa mnufaika katika mgodi huo wa Chumvi?
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang Rose kamili amesema kwenye ramani madini hayo yanaonekana yapo upande wao na sio Babati hivyo wao ndo wanufaika.
“Sasa kwa kuwa tunapitia kwao nao wanataka kunufaika,basi na mahindi na mbaazi zao wanazosafirisha wasoitishe kwetu”alisema Mwenyekiti
Mheshimiwa Kamili amesema halmashauri hiyo inakusanya ushuru wa chumvi hivyo shilingi 2000 kwa gunia ambapo kwa mwaka ni shilingi Milioni moja katika msimu huu wa mvua na kwamba pakikauka wanapata zaidi ya hapo.

About the author

mzalendoeditor