Featured Michezo

KASI YA YANGA HAIZIMIKI,YAIZAMISHA MTIBWA,MAYELE APEWA NG’OMBE

Written by mzalendoeditor

Na.Alex Sonna

VINARA wa Ligi Kuu ya NBC na Mabingwa wa Kihistoria Tanzania Timu ya Yanga wameendeleza vichapo kwa wapinzani baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar mchezo uliopigwa katika uwanja wa Manungu Turiani Morogoro.

Wakicheza mchezo wao wa 15 wa kukamilisha mzunguko wa kwanza zilianza mchezo kwa kushambuliana kwa zamu huku kosa kosa zikiendelea kutawala.

Kabla ya kwenda mapumziko Kiungo Mshambuliaji  Saido Ntibazonkiza aliwanyanyua mashabiki wake dakika ya 45+5 akifunga bao safi mara baada ya kupokea pasi kutoka kwa Fei Toto.

Kipindi cha pili kilianza kwa wenyej Mtibwa kurudi kwa kasi pamoja na kila timu kufanya mabadiliko na mnamo dakika ya 65 Mshambuliaji raia wa Congo Fiston Mayele alipingilia msumari wa pili akimalizia pasi ya Saido Ntibazonkiza.

Kwa ushindi huo Yanga wanaendelea kuongoza Ligi wakiwa na Pointi 39 wakiwaacha Simba kwa Pointi 8 huku Simba wakibaki na Pointi 31 nafasi ya pili huku Mtibwa Sugar wakibaki nafasi ya 15 wakiwa na Pointi 12 na Nafasi ya tatu Azam FC.

Baada ya mchezo kumalizika Mshabiki mmoja amemzawadia zawadi ya Ng’ombe Fiston Mayele kutokana na kuvutiwa na Mshambuliaji huyo.

About the author

mzalendoeditor