Featured Kimataifa

MAKAHAMA YA COLOMBIA YAHALALISHA UTOAJI WA MIMBA NCHINI HUMO

Written by mzalendoeditor

Wanaharakati wanaounga mkono utoaji mimba wakisheherekea uamuzi wa mahakama mjini Bogota

Colombia siku ya Jumatatu imekuwa nchi ya karibuni huko Latin Amerika kupanua ufikiaji wa fursa ya utoaji mimba wakati mahakama ya kikatiba ya taifa hilo ikipiga kura ya kuhalalisha utaratibu wa utoaji mimba hadi wiki ya 24 ya ujauzito.

Uamuzi wa mahakama yenye majaji tisa haukufikia matarajio ya makundi ambayo yalikuwa yakishinikiza utoaji mimba kuharamishwa kabisa nchini humo. Lakini hata hivyo ilielezewa kuwa tukio la kihistoria na mashirika ya kutetea haki za wanawake ambayo yanakadiria wanawake laki nne wanatoa mimba kwa siri nchini humo kila mwaka.

Kabla ya uamuzi huo Colombia iliruhusu utoaji mimba pekee wakati maisha ya mwanamke yalikuwa hatarini, au mtoto aliye tumboni alikuwa na kasoro au ujauzito uliotokana na ubakaji.

CHANZO:VOASWAHILI

About the author

mzalendoeditor