Featured Michezo

BIASHARA UNITED YAZIDI KUPAA LIGI YA NBC,YAIZAMISHA AZAM FC

Written by mzalendoeditor

WANAJESHI wa Mpaka timu ya Biashara United wamemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC mchezo uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mchezo ulianza kwa kasi kwa kila timu kutaka kupata mabao ya haraka hadi mapumziko hakuna timu iliyokuwa mbele ya mwenzake.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko hata hivyo Biashara walinufaika na mabadiliko hayo mnamo dakika ya 49 Mshambuliaji Collins Opare aliwanyanyua kwa kufunga bao safi.

Kuingia kwa bao hilo liliwaamsha Azam FC na kuanza kutafuta bao la kuwasawazisha hata hivyo ndoto zao zilizimwa dakika 90 na James Shagara.

Kwa ushindi huo Biashara united wamefikisha nafasi ya 15 na kupanda mpaka nafasi ya 12 huku Azam FC wakibaki nafasi ya 3 wakiwa na pointi 24.

Ligi hiyo inatarajia kuaendelea kesho kwa mechi moja vinara Yanga SC watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar mchezo utakaopigwa uwanja wa Manungu mjini Morogoro majira ya saa kumi jioni.

About the author

mzalendoeditor