KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA WIZI WA MIFUGO.
Mnamo tarehe 20.02.2022 majira ya saa 05:45 alfajiri huko Kitongoji cha Kasama, Kata ya Ibanda, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. SINAEL MWALAMBILA MBOTA [36] Mkazi wa Kasama aligundua kuibiwa ng’ombe wake dume, mweusi, mwenye baka jeupe ambaye thamani yake ni Tshs 800,000/= zizini nyumbani kwake. Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi lilianza msako mara moja na kufanikiwa kumkamata MANENO ESSAU SEME [30] mkazi wa Kijiji cha Kasumulu akiwa katika harakati za kutafuta mteja ili kumuuza ng’ombe huyo. Chanzo ni kujipatia kipato isivyo halali. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA KUVUNJA NYUMBA USIKU NA KUIBA.
Mnamo tarehe 20.02.2022 majira ya saa 19:00 jioni Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya Misako maeneo mbalimbali ya Jiji na Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa kumi na moja [11] wa makosa ya kuvunja nyumba usiku na wizi ambao ni:-
- VICTOR RICHARD [39] Mkazi wa Makunguru.
- JUSTINE NORBERT [19] Mkazi wa Makunguru.
- GEOFREY SIMON [20] Mkazi wa Makunguru.
- ERICK MATHEO [27] Mkazi wa Ilemi.
- JONAS BETRAM [32] Mkazi wa Makunguru.
- HENRY MWAMFUPA [28] Mkazi wa Mwanjelwa.
- ROBERT MWAKYUSA [36] Mkazi wa Iyunga.
- GOODLUCK FRANK [20] Mkazi wa Nonde.
- BENNY FREDY [26] Mkazi wa Nonde.
- SAID HAMIS [31] Mkazi wa Iganzo.
- ABDALLAH LUCAS [22] Mkazi wa Ghana.
Aidha katika upekuzi uliofanywa na Jeshi la Polisi katika makazi ya watuhumiwa walikutwa wakiwa na mali mbalimbali za wizi ambazo ni:- Mtungi wa Gas Mihan, Jiko la Gesi aina ya Boss, Diaba 01, Godoro 01, Amplifier, Simu mbalimbali za mkononi nzima na mbovu, Computer mbili, Memory card, flash disk na subwoofer ambavyo viliibwa maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya. Watuhumiwa wote wamekiri kujihusisha na vitendo vya uvunjaji na wizi. Msako wa kuwatafuta watuhumiwa wengine ambao ni wapokeaji [receivers] wa mali hizo unaendelea.
KUPATIKANA NA POMBE KALI ZLIZOKATAZWA KUINGIA NCHINI.
Mnamo tarehe 20.02.2022 majira ya saa 12:40 mchana huko Kitongoji cha Kilambo, Kata ya Njisi, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako na kufanikiwa kumkamata RUBEN ADAMU [26] Mkazi wa Kitongoji cha Lebele akiwa na pombe kali toka nchini Malawi zilizokatazwa kuingizwa nchini ambazo ni:-
- Ice Dry London Gin chupa 12 mils 200,
- Rider 200ml chupa 28,
- A1 Gin chupa 24 mls200 na
- Right Choice chupa 28 mls 200.