Featured Kimataifa

MAMA NA WATOTO WAKE WAMTEMBEZEA KICHAPO MCHEPUKO WA BABA

Written by mzalendoeditor
Jeshi la Polisi nchini Malawi, linawashikilia watu watatu wa familia moja, akiwemo mwanamke Rosina Matewere na wanaye wawili, Deus Matewere na Lydia Matewere kwa kosa la kumshambulia na kumdhalilisha mwanamke mmoja kwa kipigo, kumvua nguo na kumtembeza mbele za watu kwa madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na baba wa familia hiyo.
Video ya tukio hilo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, imezua taharuki kubwa ambapo mwanamke huyo na wanaye walijaribu kukimbia baada ya kitendo hicho lakini walikamatwa na polisi.
Jeshi la polisi nchini humo limesema halitavumilia vitendo vyovyote vya kinyama kinyume na haki za binadamu kwani kitendo cha mwanamke huyo kuvuliwa nguo na kutembezwa mbele za watu na mwanamke mwenzake kwa sababu ya wivu wa kimapenzi, kinaushushia heshima utu wa mwanamke.

About the author

mzalendoeditor