Featured Michezo

TANZIA:BEKI WA ZAMANI SIMBA AFARIKI DUNIA

Written by mzalendoeditor
BEKI wa zamani wa Simba, Adam Suleiman ’Tata’ amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwao, Tanga ambako alirudishwa kutoka Morogoro alipokuwa anaishi baada ya hali yake kuwa mbaya.
Adam Suleiman aliyeibukia Muheza Shooting akacheza pia na Reli ya Morogoro ni baba wa beki mwingine wa Simba, Miraj Adam ambaye alifuata nyayo za baba yake kwa kucheza Msimbazi.
Adam Suleiman alicheza Simba mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanawe aliibukia timu ya vijana ya Simba mwaka 2012, kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2013, lakini baada ya misimu miwili akaachwa.

Marehemu Adamu Seleman (wanne kushoto) aliyechuchumaa kwenye kikosi cha Simba mwaka1989.

About the author

mzalendoeditor