Afisa Mtendaji Mkuu Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mwanaidi Mohammed Ali akizungumza na Waandishi wa Habari kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mama Maryam Mwinyi kuhusu uzinduzi wa Taasisi ya Zanzibar Maisha bora Foundation unaotarajiwa kufanyika febuari 19.2022 katika Uwanja vya Mao Zedong Mjini Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.
…………………………………………………..
Na Mwashungi Tahir Maelezo
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi anatarajia kuzindua Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation kwa ajili ya kuwajali na kuwashajihisha makundi mbali mbali wakiwemo wanawake, vijana na watoto ikiwa ni azma ya Serikali katika kuwakuza kiuchumi wananchi wake .
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Wizara ya Utalii Kikwajuni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasis hiyo Mwanaidi Mohammed Ali kwa niaba ya Mama Mwinyi amesema Taasisi hiyo itazinduliwa tarehe 19/2/2022 siku ya jumamosi katika Uwanja wa Mao zedong
Amesema katika uzinduzi huo kutafanyika matembezi kuanzia Kiembesamaki Butros kupitia barabara ya Mazizini, Kilimani chini , Miembeni, Michenzani hadi kumalizia Uwanja wa Mao ze dung na kutolewa huduma mbali mbali za uangalizi wa afya kwa wananchi wote.
Aidha amefahamisha kuwa huduma zitakazotolewa hapo za afya ni pamoja na kupima sukari, kupima uzito, kuchangia damu, kufanyiwa uchunguzi wa macho, kupata chanjo ya UVIKO 19. Meno na baadhi ya maradhi mengine ambazo huduma hizo zote zitatolewa bure.
Pia amesema matembezi hayo yatapofanyika wananchi wajitokeze kwa wingi na kwa wale watakaokuwa hawawezi kwenda sehemu zote wanaruhusiwa kukaa barabarani au hata kusubiria hapo kwenye kiwanja cha Mao zedong ni kumuunga mkono mama Mwinyi.
“Ikiwa mwananchi hawezi matembezi hayo kupita sehemu zote zilizotajwa anaweza kukaa barabarani au kuyangojea huko kwenye uwanja wa mao de zung ili na wao waweze kushiriki”, alisema mama Mwinyi.
Akizungumzia upimaji wa uviko 19 Mama Mariam amewasisitiza wananchi kupata chanjo kwani maradhi bado yapo hivyo endapo wananchi watajitokeza kupatiwa chanjo hiyo itasaidia kupunguza ukali wa maradhi hayo ambayo yameshamiri duniani kote.
Mama Mariam Mwinyi ameanzisha Taasisi hiyo kwa lengo la kuwaweka akinamama hasa wanaolima mwani kuwaunga mkono na kuimarisha uchumi wa buluu.