Featured Michezo

LIVERPOOL YANG’ARA UGENINI DHIDI YA INTER MILAN LIGI YA MABINGWA ULAYA

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Liverpool imetanguliza mguu mmoja Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Inter Milan usiku wa Jumatano Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan nchini Italia.
Katika mchezo huo wa kwanza Hatua ya 16 Bora, mabao ya Liverpool yamefungwa na Roberto Firmino dakika ya 75 na Mohamed Salah dakika ya 83.
Mechi nyingine ya 16 Bora jana, wenyeji, Red Bull Salzburg wamelazimishwa sare ya 1 -1 na Bayern Munich Uwanja wa Red Bull Arena Jijini Wals-Siezenheim.

About the author

mzalendoeditor