OFISI ya Rais TAMISEMI inafanya tathimini nchi nzima ili kuangalia namna bora ya matumizi ya fedha za asilimia 10 za halmashauri kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Haya yameelezwa Bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali, Mhe. Innocent Bashungwa wakati akitoa ufafanuzi kutokana na swali la nyongeza la Mbunge wa Vunjo, Charles Kimei
Alisema tathimini ya awali inaonesha kuwa zaidi ya Sh bilioni 60 kila mwaka zinakusanywa na kutengwa kwenye halmashauri kwa ajili ya mikopo hiyo.
” Kwa hiyo tungependa kuona mabilioni haya yanakwenda kwenye vikundi yanaleta tija yanasaidia vikundi ambavyo pia vinasaidia katika kujenga uchumi nchi. Baada ya kukamilisha tathimini na kufanya uchambuzi tutaleta bungeni ili muweze kutushauri ili tuweze kwenda vizuri.”
Mbunge Kimei alitaka kujua kama Ofisi ya Rais-TAMISEMI haioni umuhimu wa kuziwezesha halmashauri kutenga maeneo mahususi kwa wajili ya wajasiliamali na kuyawekea miundombinu stahiki ili wanufaika wa fedha za asilimia 10 za halmashauri wakatumia maeneo hayo kufanya shughuli zao.
Pia alitaka kujua kama Wizara haioni haja ya kushirikiana na SIDO kwenye utoaji wa mikopo ya halmashauri hasa ikizingatia kuwa fedha zinazokopewa na SIDO zimekuwa zikirejeshwa Kwa zaidi ya asilimia 90.
Akijibu maswali hayo, Bashungwa alisema ni la Zima Halmashauri kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya uwekezaji na vikundi vinavyokopa asilimia 10 ya fedha za halmashauri kuwa Moja wa wanufaika wa maeneo hayo.
“Mhe Mbunge(Charles Kimei) tukuhakikishie hili tumeboresha zaidi, tumeshaka na Wizara ya Kilimo kuangalia makundi ya vijana wasomi ambao wanapata asilimia 10 ya fedha za halmashauri zetu, majiji na manispaa namna bora ya kuweza kuwasaida maeneo mahususi kama haya. Hoja kama hii tunaifanyia kazi.”