Featured Michezo

TAZAMA MASHABIKI WA YANGA WALIVYOCHEZEA KICHAPO KWA MKAPA

Written by mzalendoeditor

Kabla ya mechi ya Simba na Asec Mimosas kuanza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Mashabiki wa Simba wamewahamisha maeneo ya kukaa baadhi ya mashabiki waliosadikika kuwa wa Yanga.

Mashabiki hao walionekana kuvalia jezi za timu zao za njano na kijani huku wakionekana kushangilia kwa staili ya ‘Kuwajaza’ inayotumiwa na mshambuliaji wa timu hiyo Heritier Makambo.

Mashabiki wa Simba waliwafuata na kuwaondosha kwa nguvu na baadhi kuwapiga katika majukwaa waliyokuwa wakiimba nyimbo hizo.

Baada ya hapo mashabiki hao waliondoka mara moja maeneo hayo na kutafuta sehemu ambazo hazina mashabiki wengi wa Simba.

About the author

mzalendoeditor