……………………………………………..
WAWAKILISHI Pekee ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Timu ya Simba wameanza vyema katika Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuichapa mabao 3-1 Asec Mimosas kutoka Ivory Coast mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Papa Sakho aliwainua mashabiki wa Simba dakika ya 12 akifunga bao kwa Acrobatic akipokea pasi ya Shomari Kapombe hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kushambuliana kwa zamu mnamo dakika ya 60 Stephane Aziz Ki aliisawazishia timu yake ya Asec Mimosas baada ya kusawazisha wenyeji walianza kulishambulia lango la wageni kama nyuki.
Dakika ya 79 Simba walipata penalti iliyofungwa na Shomari Kapombe baada ya mlinda mlango Abdoul Cisse kumchezesha madhambi Yussuph Mhilu ndani ya 18.
Simba waliendelea kuliandama lango la Asec winga hatari kutoka Malawi Peter Banda alipigilia msumari wa tatu dakika ya 81 akimalizia mpira wa John Bocco.
Kwa ushindi huo Simba wanaongoza Kundi D kwa Pointi tatu na mchezo mwingine wa kundi hilo RSB Berkane watakuwa nyumbani majira ya saa nne kucheza na US Gendarmerie.