Featured Kitaifa

MBUNGE CHIKOTA AFUNGUKA UHABA WA WALIMU, WATUMISHI WA AFYA

Written by mzalendoeditor

MBUNGE wa Nanyamba(CCM),Abdallah Chikota ameiomba serikali kutoa kibali maalum cha kuajiri walimu na watumishi wa kada ya afya kutokana na kuwepo kwa uhaba mkubwa wa watumishi hao nchini.

Chikota amesema hayo bungeni alipokuwa akichangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Amesema kutokana na hali ilivyo kwenye Halmashauri baada ya kujengwa miundombinu ya madarasa na vituo vya afya ni vyema serikali ikachukua hatua za makusudi kuajiri watumishi wa sekta hizo.

“Kazi kubwa ambayo imefanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ya ujenzi wa madarasa 15,000, vituo vya afya, faida za ujenzi wa miundombinu hii haitaonekana kama upungufu huu ukiendelea naomba serikali ichukue hatua za makusudi kutoa kibali maalum kwa ajili ya kuajiri walimu na watumishi wa sekta ya afya.”

“Naiomba serikali yangu sikivu itoe kibali maalum kama ilivyofanya miaka ya nyuma tulivyokuwa na uhaba wa wahasibu,”amesema.

About the author

mzalendoeditor