Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali ya awamu ya sita tayali imepeleka Bilioni 30 kwenye mikoa 10 ambapo kila mkoa umepokea sh. Bilion 3 kwa ajiri ya kujenga shule maalum za sayansi kwa ajili ya wanafunzi wa kike.
Waziri Bashungwa ameeleza hayo katika mdahalo maalum wa kujadili mafaniko katika Sekta ya elimu kwa mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani uliofanyika kwa njia ya mtandao wa Zoom Februari 12, 2022.
Waziri Bashungwa amesema kupitia mradi wa SEQUIP Serikali imepeleka Bilioni 110 kwenye kata 235 ambazo hazina shule za Sekondari na ujenzi umeshaanza na wengine wapo hatua ya ukamilishaji wa shule hizo 235.
Aidha, Waziri Bashungwa ameeleza kuwa ndani ya utawala Rais Samia Suluhu Hassan tayalri ameshatoa kibali cha kuajiri Walimu 6949 ambapo Walimu 3000 walikuwa Walimu wa sayansi kwa shule za Sekondari.
Pia, ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuzielekeza fedha za mkopo wa IMF katika miradi endelevu na inayoonekana kama ujenzi wa madarasa 12,000 ambayo yamepunguza msongamano madarasa na wanafunzi kutembea mwendo mrefu.
Pamoja na mafanikio hayo, Waziri Bashungwa ameeleza kuwa Wizara imeomba kibali kwa Mheshimiwa Rais aridhie ajira za Walimu 7,000 ili kupunguza upungufu wa walimu kawa shule za msingi na sekondari.
Vile vile, Waziri Bashungwa amebainisha kuwa kupitia bajeti inayondaliwa kwa mwaka 2022/ 23 wataweka kipaumbele cha kukabili upungufu wa matundu ya vyoo hasa kwa shule za msingi itakayokwenda sambamba na kupunguza nyumba za walimu.