WENYEJI, Dodoma Jiji FC wamechapwa mabao 2-1 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Kagera Sugar inayopata ushindi wa kwanza baada ya mechi sita yote yamefungwa na mshambuliaji Hassan Mwaterema dakika ya 31 na 76, wakati la Dodoma Jiji limefungwa na Issa Abushehe dakika ya 67.
Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 13 katika mchezo wa 12 na kujiinua kutoka mkiani hadi nafasi ya 10, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 17 za mechi 13 nafasi ya saba.