Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Mohamed Omar, Novemba 12, 2025, jijini Dar es Salaam, amezindua Mpango wa Utekelezaji Mwongozo wa kuwarejesha shule wanafunzi waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali, hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa elimu inapatikana kwa kila mtoto nchini.
Dkt. Omar ameeleza kuwa Mpango huo ni muhimu na utatoa dira kwa Serikali na wadau elimu katika kutekeleza kikamilifu sera ya elimu na Mwongozo wa urejeshaji ili kuhakikisha kuwa watoto wote, bila kujali changamoto walizokutana nazo, wanapata nafasi ya kuendelea na masomo yao.
“Watoto wetu wa kike na wa kiume, wanapokatisha masomo, si mwisho wa maisha yao, kuna fursa zaidi ya elimu ili kufikia malengo yao na waweze changia maendeleo ya taifa kwa ujumla” amesisitiza Dkt. Omar.
Aidha ameupongeza Mtandao wa Elimu Tanzania(TENMET) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) pamoja na wadau mbalimbali wa elimu katika kufanikisha utekelezaji wa mkakati huo unaolenga kutoa fursa sawa kwa watoto wote katika ngazi ya elimu ya msingi na sekondari.
Katika hatua ingine Dr Omar pia amezindua taarifa ya utafiti uliofanyika juu ya utekelezaji Mwongozo wa urejeaki kwa kundi moja wa wanafunzi wa kike waliokatisha masomo kutokana na ujaouzito.
Taarifa hiyo inaelezea mafanikio makubwa ambayo yam-ewezesha wanafunzi wa kike zaidi 13,000 na wa kiume 17,000 kurejea kuendelea na masomo.
