Featured Kitaifa

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAWASILISHA TAARIFA YA MAJUKUMU KWA KAMATI YA BUNGE

Written by Alex Sonna

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepokea na kujadili taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Taasisi zilizo chini yake.

Kamati hiyo, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, imepokea taarifa hiyo leo Januari 21, 2026, Bungeni jijini Dodoma, ambapo iliwasilishwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainab Katimba (Mb).

Akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa hiyo, Mhe. Katimba ameieleza Kamati kuhusu majukumu ya Wizara kwa mujibu wa hati idhini iliyotolewa katika gazeti la serikali Na.686 la tarehe 19 Desemba, 2025.

About the author

Alex Sonna