Featured Kitaifa

MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA MAWAKALA WA FORODHA YAKAMILIKA

Written by mzalendoeditor

Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Mawakala wa Fordha yamekamilika huku viongozi wa sekta mbalimbali wakitarajiwa kushiriki katika kujadili njia bora za kuimarisha mifumo ya forodha na kuhimiza biashara ya kimataifa. Mkutano huo, unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 30 April mpaka tarehe Mosi Mei,2025 kwenye Hotel ya Golden Tulip, Zanzibar , utaangazia masuala ya teknolojia ya kisasa katika forodha, uwazi wa mchakato wa biashara, na mikakati ya kudhibiti magendo.

Akizungumza na Wanahabari Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar Mhe Idrissa Kitwana Mustapha ametoa pongezi kwa kamati za maandalizi kutoka Tanzania Bara na Visiwani kwa kazi nzuri na kuhimiza washiriki kutumia fursa hiyo kujenga ushirikiano imara na kuleta mapendekezo yatakayoharakisha maendeleo ya sekta ya forodha nchini.

Mkutano huu unatarajiwa kuvutia wadau zaidi ya 500 kutoka sekta za umma na binafsi, pamoja na washirika wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

About the author

mzalendoeditor