Featured Kitaifa

MAELEKEZO SABA YA WAZIRI MCHENGERWA KWA WAKUU WA MIKOA NCHINI

Written by mzalendo

Na Gideon Gregory, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ametoa maelekezo Saba kwa wakuu wa mikoa nchini kuwasimamia wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa kuzingatia vipaumbele mbalimbali ikiwemo kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unafikia malengo.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio ya mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais- TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2025/26.

“Maelekezo mengine ni kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya afya ya msingi, elimumsingi na sekondari kulingana na mipango iliyowekwa,”amesema.

Adha, amesema amewaelekeza wasimamie utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Uchumi wa Kidigitali ikiwemo uwekaji na matumizi ya mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa ikiwa ni pamoja na vituo vya huduma za afya na elimu.

“Kuhakikisha mapato katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa yanakusanywa kupitia mifumo ya TEHAMA ya Serikali pamoja na kufanya ufuatiliaji wa karibu wa mifumo hiyo ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato,”amesema.

Katika hotuba yake Waziri Mchengerwa ameliomba Bunge likubali kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2025/26 yenye jumla ya shilingi Trilioni 11.7 kwa ajili hiyo na taasisi zilizo chini yake.

About the author

mzalendo