Featured Kitaifa

MAHAFALI YA PILI YA CHUO KIKUU CHA THERAPON SHINYANGA YAFANYIKA

Written by mzalendoeditor
Sehemu ya wanafunzi waliohitimu masomo ya dini ya Kikristo ya Theolojia katika ngazi tofauti.
Na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Mahafali ya Pili ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga yamefanyika ambapo wanafunzi 10 wamehitimu masomo ya dini ya Kikristo ya Theolojia katika ngazi tofauti, ikiwa ni pamoja na Shahada ya Awali (Bachelor), Stashahada ya Uzamili (Post Graduate Diploma), na Shahada ya Umahiri (Master). Hii ni hatua muhimu katika maendeleo yao ya kiroho na kitaaluma, na inawakilisha mchango mkubwa katika huduma za kiroho na jamii zao.
Mahafali hayo ya pili yamefanyika leo Jumamosi Oktoba 26,2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Therapon Tanzania Dkt. Emmanuel Joseph Makala ambaye ni Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria.
Katika hotuba yake wakati akiwatunuku Shahada Watumishi wa Mungu wachungaji, wainjilisti na wazee wa kanisa ambao wamehitimu masomo yao bora ya theolojia katika nyanja mbali mbali kwenye Chuo Kikuu cha Therapon, tawi la Tanzania, Mkuu wa Chuo hicho Askofu Mstaafu, Dkt. Makala amewataka wahitimu kutumia elimu waliyopata kuwafundisha wengine kuhusu Neno Sahihi la Mungu, akirejelea kifungu cha Biblia cha Mathayo 28:19-20.
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari,” amesisitiza Dkt. Makala, akiongeza kuwa wahitimu wanapaswa kuibadilisha dunia kwa kutumia maarifa waliyopata.
Mkuu wa Chuo  Kikuu cha Therapon (Kampasi ya Tanzania) Askofu Mstaafu Dkt. Emmanuel Joseph Makala
Dkt. Makala amekemea mmomonyoko wa maadili, akihamasisha umuhimu wa kuzuia ndoa za jinsia moja, akisema ni upotoshaji wa maadili.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mafunzo Chuo Kikuu cha Therapon (Kampasi ya Tanzania) Therapon University – Tanzania, Dkt. Kulwa Meshack amewataka wahitimu hao wakawe chumvi na nuru ya ulimwengu akiwasisitiza kuihubiri Injili takatifu ya Mungu na kulifundisha Neno la Mungu kwa usahihi wote.
“Maombi yangu kwenu ni kwamba, kama Yesu Kristo alivyowaita katika utumishi wake mtakatifu, hivyo nendeni mkawe chumvi na nuru ya ulimwengu. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu na uweza wake, mkajikite katika kuihubiri Injili takatifu ya Mungu na kulifundisha Neno la Mungu kwa usahihi wote hivyo kusababisha matokeo chanya kwa kanisa la Kristo na ulimwenguni”,amesema Dkt. Meshack.
Mratibu wa Mafunzo Chuo Kikuu cha Therapon (Kampasi ya  Tanzania), Dkt. Kulwa Meshack 
“Hakikisheni pia mnatoa mchango chanya kwenye dunia ya sasa iliyojaa mmonyoko wa maadili kuanzia katika ngazi ya mtu mmoja mmoja na familia. Changieni katika kupunguza changamoto za unyanyasaji wa aina zote. Msisukumwe hasa na nguvu ya mapato bali wito mtakatifu mlioitiwa na Mungu hata kama kwa kufanya hivyo hamtapata mapato makubwa katika utumishi wenu. Pato kuu liwe taji ya wokovu na ya utumishi mwema mbele za Mungu”,ameongeza Dkt. Meshack.
Akifafanua zaidi Dkt. Meshack amesema Therapon University – Tanzania ni Chuo Kikuu cha masafa (open and distance learning), cha kikristo kilichosajiliwa na taasisi mbili kubwa za Kikristo nchini Marekani.
Sehemu ya wanafunzi waliohitimu masomo ya dini ya Kikristo ya Theolojia katika ngazi tofauti.
“Usajili huu unathibitisha kuwa elimu na vyeti vilivyotolewa leo vinataambuliwa na vyuo vikuu vya Kikristo nchini Marekani chini ya Shirikisho hili, pamoja na vyuo vya kikristo vilivyoko Afrika vilivyosajiliwa na Acreditation of Theological Education in Africa (ACTEA), na mashirikisho mengine duniani.
 
Pamoja na uhakika wa usajili wa chuo hiki, chuo kimejikita katika kutengeneza wahitimu bora kabisa na wabobezi katika nyanja za Theolojia (theology), Elimu ya Utumishi wa Kikristo (Divinity), Elimu ya Kikristo (Christian Education), Uongozi na Utawala wa Kikristo (Christian Leadership and Management), Ushauri na Saikolojia ya Kikristo (Christian Counseling and Psychology), Urejeshwaji wa Haki (Restorative Justice), na Utetezi wa Imani ya Kikristo (Christian Apologetics), na Huduma za Kikristo (Christian Ministries), na Kazi za Kijamii kwa mlengo wa Kikristo (Christian Social Work)”,ameongeza Dkt. Meshack.
Ameeleza kuwa, katika utoaji wa elimu hiyo wana mashirikiano ya Therapon University – Tanzania kitaaluma na Chuo Kikuu cha Therapon, Scofield Graduate School cha Marekani Trinity Graduate School of Apologetics and Theology cha nchini India.
Kwa upande wake Mtaaluma Mkuu, Chuo Kikuu cha Therapon (Kampasi ya Tanzania) Dkt. Emmanuel Buganga amesema katika kundi la wahitimu 10, wanne wamepata Shahada ya Kwanza, mmoja Stashahada ya Uzamili na watano Shahada ya Umahiri, wakifanya utafiti katika nyanja tofauti za Theolojia.
Mtaaluma Mkuu, Chuo Kikuu cha Therapon (Kampasi ya Tanzania) Dkt. Emmanuel Buganga.
Wahitimu Shahada ya Kwanza ni Juma Mwesigwa Mohamed (Shahada ya Kwanza ya Theolojia katika Utawala wa Taasisi na Uongozi wa Kimkakati) – Bachelor of Theology in Organization Leafership & Strategic Management  ,  Nakhomowa Richard Mlade (Shahada ya Kwanza ya Theolojia) Bachelor of Theology, Musa Isaya Majama (Shahada ya Kwanza ya Theolojia katika Utawala wa Taasisi na Uongozi wa Kimkakati) – Bachelor of Theology in Organization Leafership & Strategic Management na Milca Kakete Shahada ya Kwanza ya Theolojia katika Ushauri wa Kikristo (Bachelor of Theology in Christian Counseling)
Aliyehitimu Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) ni Amos Abdallah Shija Stashahada ya Uzamili katika Elimu ya Kikristo (Postgraduate Diploma in Christian Education).
Amefafanua kuwa Waliohitimu shahada ya Umahiri (Master) ni Charles Yakobo Mashenenhe (Shahada ya Umahiri wa Theolojia katika Uongozi na Utawala wa Kimkakati) – Master of Theology in Christian Strategic Leadership and Management, Utafiti: “Ujenzi Mpya wa Urathibiti wa Maisha ya Kikristo” (Reconstruction of Spiritual Life Management); Emmanuel Njoka Suleiman (Shahada ya Umahiri katika Utumishi) – Master of Theology in Divinity, Utafiti: “Ufafanuzi wa 1 Yohana” (Commentary of 1 John): Reuben Jeremia Suluba (Shahada ya Umahiri katika Ushauri wa Kikristo) Master of Theology in Christian Counseling, Utafiti: “Ushauri wa Kiafrika katika Mtazamo wa Kibiblia African Counseling in Biblical Perspective.
Wengine ni Sospenous M. R. Mabele (Shahada ya Umahiri katika Ushauri wa Kikristo) Master of Theology in Christian Counseling), Utafiti: “Mtazamo wa Kibiblia kuhusu Mchepuko katika Ndoa za Kikristo” Biblical Perspective on Extra-marital Relationship in Christian Marriages, na Thomas Kundael Sam (Shahada ya Umahiri wa Theolojia katika Uongozi na Utawala wa Kimkakati) – Master of Theology in Christian Strategic Leadership and Management, Utafiti: “Mgogoro wa Kimaslahi katika Makanisa” (Conflict of Interest in Churches).
Mkuu wa Chuo  Kikuu cha Therapon (Kampasi ya Tanzania) Askofu Mstaafu Dkt. Emmanuel Joseph Makala (kulia) akimpongeza Juma Mwesigwa Mohamed wakati akimtunuku Shahada ya Kwanza ya Theolojia katika Utawala wa Taasisi na Uongozi wa Kimkakati) – Bachelor of Theology in Organization Leafership & Strategic Management
Nao Wahitimu wametoa shukrani kwa chuo kwa elimu waliyoipata, wakisema ni hazina kwa ajili ya kazi ya Mungu.
 
“Elimu hii imepanua ufahamu wetu na itatumika katika kulielimisha kanisa,” wamesema.
Mahafali haya yanasherehekea mafanikio ya wahitimu na kuwakumbusha juu ya wajibu wao katika kutumikia jamii na kanisa kwa ufanisi.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Chuo  Kikuu cha Therapon (Kampasi ya Tanzania) Askofu Mstaafu Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza leo Jumamosi Oktoba 26,2024 wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga ambapo wanafunzi 10 wamehitimu masomo ya dini ya Kikristo ya Theolojia katika ngazi tofauti, ikiwa ni pamoja na Shahada ya Awali (Bachelor), Stashahada ya Uzamili (Post Graduate Diploma), na Shahada ya Umahiri (Master). – Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkuu wa Chuo  Kikuu cha Therapon (Kampasi ya Tanzania) Askofu Mstaafu Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza leo Jumamosi Oktoba 26,2024 wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga

Mratibu wa Mafunzo Chuo Kikuu cha Therapon (Kampasi ya  Tanzania), Dkt. Kulwa Meshack akizungumza wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Mratibu wa Mafunzo Chuo Kikuu cha Therapon (Kampasi ya  Tanzania), Dkt. Kulwa Meshack akizungumza wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Mtaaluma Mkuu, Chuo Kikuu cha Therapon (Kampasi ya Tanzania) Dkt. Emmanuel Buganga  akizungumza wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga
Mkuu wa Chuo  Kikuu cha Therapon (Kampasi ya Tanzania) Askofu Mstaafu Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza leo Jumamosi Oktoba 26,2024 wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo Kikuu cha Therapon (Therapon University) Kampasi ya Shinyanga. Kushoto ni Mtaaluma Mkuu, Chuo Kikuu cha Therapon (Kampasi ya Tanzania) Dkt. Emmanuel Buganga , kulia ni  Mratibu wa Mafunzo Chuo Kikuu cha Therapon (Kampasi ya  Tanzania), Dkt. Kulwa Meshack
Sehemu ya wanafunzi waliohitimu masomo ya dini ya Kikristo ya Theolojia katika ngazi tofauti, ikiwa ni pamoja na Shahada ya Awali (Bachelor), Stashahada ya Uzamili (Post Graduate Diploma), na Shahada ya Umahiri (Master). 

Mkuu wa Chuo  Kikuu cha Therapon (Kampasi ya Tanzania) Askofu Mstaafu Dkt. Emmanuel Joseph Makala akimtunuku Juma Mwesigwa Mohamed  (kushoto) Shahada ya Kwanza ya Theolojia katika Utawala wa Taasisi na Uongozi wa Kimkakati) – Bachelor of Theology in Organization Leafership & Strategic Management 
 Mratibu wa Mafunzo Chuo Kikuu cha Therapon (Kampasi ya  Tanzania), Dkt. Kulwa Meshack akimkabidhi cheti Juma Mwesigwa Mohamed (kulia) wakati akitunukiwa Shahada ya Kwanza ya Theolojia katika Utawala wa Taasisi na Uongozi wa Kimkakati) – Bachelor of Theology in Organization Leafership & Strategic Management 
Mkuu wa Chuo  Kikuu cha Therapon (Kampasi ya Tanzania) Askofu Mstaafu Dkt. Emmanuel Joseph Makala  (kulia) akiendelea kuwatunuku shahada wahitimu

Picha za kumbukumbu
Picha za kumbukumbu
Picha za kumbukumbu
Burudani ikiendelea
Burudani ikiendelea
Burudani ikiendelea
Burudani ikiendelea
Wageni waliodhuria mahafali hayo
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

About the author

mzalendoeditor