Featured Kitaifa

KANISA LA AICT WAUNGA MKONO AGENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Written by mzalendoeditor

DAR ES SALAAM – AICT

Kanisa la Uaskofu la AICT Pastorate ya Magomeni  Dayosisi ya Pwani lililopo Jijini Dar es Salaam limetoa msaada wa Mitungi ya Gesi 20 kwa akina mama wanaoishi maeneo jirani na Kanisa hilo ikiwa sehemu ya shamrashamshara kuelekea Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 ya Kanisa hilo.

Msaada huo umetolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania AICT  Musa Massanja Mwangwesela ambaye pia ni Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Mwanza ambapo amesema kuwa kutolewa kwa msaada huo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania juu ya utunzaji wa Mazingira kupitia Nishati Safi ya kupikia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa shina Namba 3 Makubusho Suleimani ally Mohamed amelishukuru Kanisa hilo pamoja na Viongozi wa Kanisa hilo kwa wema wao wa kutoa msaada wa Nishati hiyo ya kupikia katika Mtaa wa Uwarani na Maswa.

Nao baadhi ya Wanufaika wa Msaada huo akiwemo  Judith Kobelo na Mariamu Gumbo wameshukuru kwa kupewa msaada huku wakisema Nishati hiyo itakavyokwenda kurahisisha upatikanaji wa Nishati hiyo safi ambayo wamekabidhiwa.

Kilele cha maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 ya Kanisa la Uaskofu la AICT Pastorate ya Magomeni  Dayosisi ya Pwani lililopo Jijini Dar es salaam ni Tarehe 27/10/2024, Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

About the author

mzalendoeditor