Featured Kitaifa

IGP WAMBURA AKAGUA MIRADI YA UJENZI RUFIJI

Written by mzalendo

Matukio mbalimbali Pichani yakimuonesha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura, akikagua Mradi wa Ujenzi wa jengo la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji ambalo ujenzi wake bado unaendelea.

Baada ya ukaguzi huo IGP Wambura pia alizungumza na maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali ambapo aliwataka kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi kwa kuzingatia nidhamu, weledi, uadilifu na kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa mteja wa Ndani na Nje sambamba na utekelezaji wa maelekezo ya Tume ya Haki Jinai.

About the author

mzalendo