Featured Kitaifa

KIKAO CHA KUTATHIMINI MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA CHAFANYIKA JIJINI TANGA

Written by mzalendo


Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Imani Clemence akizungumza wakati wa kikao cha kutathimini na kujadili utendaji wa Programu ya Utekelezaji wa Mradi wa Afya Hatua iliyopo chini ya Shirika la THPS na kufadhiliwa na Pepfar CDC kilichofanyika Jijini Tanga na kuhusisha wadau mbalimbali Mkoani Tanga wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya kutokana na mkoa huo kushika nafasi ya pili kwa watumiaji kitaifa.


Mkurugenzi Mshirika wa Huduma za Jamii –Huduma za Kinga (THPS) Dkt Appolinary Bukuku akizungumza katika kikao hicho





Afisa kutoka Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Kaskazini Sara Ndaba akizungumza jambo wakati wa kikao hicho






Na Oscar Assenga, TANGA.

KIKAO cha kutathimini na kujadili utendaji wa Programu ya Utekelezaji wa Mradi wa Afya Hatua iliyopo chini ya Shirika la THPS na kufadhiliwa na Pepfar CDC umefanyika leo Jijini Tanga na kuhusisha wadau mbalimbali Mkoani Tanga wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya kutokana na mkoa huo kushika nafasi ya pili kwa watumiaji kitaifa.

Lengo kubwa la kuwaida wadau wa utoaji wa huduma za methadone kwa waraibu za Kulevya mkoani humo pia kilikuwa na lengo la kupitia na kujadili mafanikio ya utoaji wa methadone kwa waraibu na kujadili changamoto zinazoikabili huduma hiyo na kutengeneza mikakati ya kuboresha huduma kwenye mkoa huo.

Wadau wengine walioshiriki kwenye kikao hicho ni kutoka wizara ya Afya,wawakilishi wa Timu za wasimamizi za Afya ngazi ya mkoa na Halmashauri,Jeshi la Polisi,Asasi za Kiraia zinazowaibua waraibu wa dawa za kulevya na wadau wa THPS wanaoshirikiana na serikali katika kutoa huduma na kuziboresha katika kutoa mafunzo ya huduma za methanone ,wanasaidia vifaa mbalimbali vya kazi ,watumishi ,vikao ,wanajivunia mafanikio yaliyopo leo hii waraibu

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Imani Clemence alisema Serikali kushirikiana na wadau CDC kupitia THPS imeweka nguvu kubwa kuboresha huduma za waraibu kuhakikisha wanapata huduma bora ili afya za ziweze kuimarika na wafikie hali ambayo wanaweza kuisha maisha ya kawaida na kushiriki kujenga uchumi.

Alisema kwamba hadi kufikia Mwezi Mei 2023 Mkoa wa Tanga ulikuwa na waraibu 1094 ambao walishawahi kuanzishiwa Methadone na kati yao 683 ndio ambao bado wanaendela na dawa hao wengine wapo wapi wengine wahama na wengine wamefariki.

Alisema kwamba kwa kushirikiana na wadau CDC na Shirika la THPS wametoa mchango mkubwa na Serikali inatambua juhudi zao kwenye mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi na huduma kwa waraibu .

“Tutaendelea kuwapa ushirikino katika miradi inayoendelea kutekelezwa mkoani Tanga sisi tupo tayari kuwapa ushirikiano wa kutosha wakati wote mtakapokuwa mkiitaji na niwashukuru wadau wote tushirikiana nao kwenye pambano dhidi ya dawa za kulevya”Alisema

Awali akizungumza Mkurugenzi Mshirika wa Huduma za Jamii –Huduma za Kinga (THPS) Dkt Appolinary Bukuku alisema wanajadili changamoto za huduma za waraibnu wao kama sehemu ya wadau ili waweze kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi kwa jamii ya watanzania hasa huduma wanazozitoa za waraibu kwenye mkoa wa Tanga.

Alisema wamekusanyika na wadau mbalimbali hivyo kila mdau kuitwa ni muhimu kuchangia namna bora ya kuhakikisha huduma za waraibu walioathirika na dawa za kulevya zinakwenda vizuri na watapata watu wakaokwenda kufanya kazi kwenye jamii na kuchangia pato la taifa kama watanzania.

“tunatambua kuna watu wameingia huko na walikuwa na uwezo wa kufanya kazi kama sisi lakini kutokana na athari walizokutana nazo wameshindwa kufanya kazi na kutengwa na jamii huduma hizo zilikuwa zinatolewa na Serikali na wadau zitawasdia kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuchangia pato la Taifa”Alisema

Hata alisema wamekutana wao kama wadau wakiwa na asasi za kijamii na watu wanaotoa huduma kwenye kliniki za MAT lengo likiwa kupata changamoto kutoka wa wanufaika wa huduma pamoja na kusikia changomoto kwa wale wanaowahudumia.

“Sisi sote kwa umoja wetu tuweze kutoa mchango wa kuboresha hasa zile Asasi ambazo zinawaibua,vyombo vya ulinzi ambavyo vinawachukulia kama wahalifu lakini tunatambua jamii imewatenga na kuwaona watu ambao hawafai na wao wanawajibu wa kutoa elimu kwa jamii ili wawahudumie kwa upendo ili warudi kwenye hali ya kawaida tunaishuku mamlaka wanajitahidi zao“Alisema

Naye kwa upande wake Afisa kutoka Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Kaskazini Sara Ndaba alisema kwamba wanaishukuru Shirika la la (THPS) kwa kuandaa kikao hicho cha wadau kwani wamekuwa wakiwasadia kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya.

Alisema katika kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Dini,Jeshi la Polisi,Jeshi Magereza na Wizara ya afya wote wanapambana kwenye vita dhidi ya dawa za kulevya na mkoa umethirika na dawa za kulevya.

Hata hivyo alisema kwamba uwepo wao utasaidia kukabiliana na tatizo hilo na Tanga ikaondokana na tatizo la dawa za kulevya kwa maana hali bado so shwari kutokana na kwamba kituo cha Mat kinahudumia waraibu zaidi watu 1,113 mpaka sasa kutoka kwa Asasi za kiraia ambazo zimekuwa zikiwaibua na kuwapeleka kwenye kituo .

About the author

mzalendo