Featured Kitaifa

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDO MBINU YA ELIMU

Written by mzalendo

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Mhe. Zainabu Katimba (Mb) amsema serikali inatambua umhimu na itaendelea kuboresha miundombinu ya Elimu ikiwemo Mabweni ya Wanafunzi, Uzio, Majengo ya Utawala na Mabwalo kupitia Miradi mbalimbali.

Mhe. Katimba amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu, wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini Mhe. Mhe.Reuben Kwagilwa (Mb) aliyetaka kujua, Je ni lini Serikali itajenga Bwalo la chakula, Majengo ya Utawala na Mabweni ya Wanafunzi katika Shule ya Sekondari Misima na Handeni?

“Kwa kutambua umhimu mkubwa sana wa Miundombini hii katika Shule zetu, Serikali itaendelea kutenga Fedha kwenye Bajeti kwaajili ya kuendelea kujenga Miundombinu ya Bwalo, Majengo ya utawala, Mabweni ya Wanafunzi, Uzio na mengine katika Shule za Sekondari kote Nchini zikiwemo Shule za Sekondari Misima na Handeni kupitia Miradi mbalimbali ya Elimu” Mhe. Katimba.  

Aidha Mhe. Katimba amesema Serikali inajenga Shule 26 za Bweni za wasichana za Kitaifa katika Mikoa yote Nchini kupitia Mradi wa Sequip kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilijengwa katika Mikoa kumi na Awamu ya pili zitajengwa katika Mikoa kumi na sita huku zikigharimu Jumla ya shilingi Bilioni 4.1.

Mhe. Katimba amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mhe. Innocent Edward Kalogeris (Mb) aliyeuliza, Je ni lini Serikali itajenga Shule Maalumu ya Sekondari ya Wasichana Dutumi katika Kata ya Bwakila, Morogoro vijijini?.

About the author

mzalendo