Kitaifa

DKT. MFAUME AELEKEZA UONGOZI WA MLELE KUANZA KUTUMIA MASHINE ZA LAUNDRY

Written by mzalendo

Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais -TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume ameuelekeza uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Mlele hadi kufikia mwisho wa mwezi Machi mashine zilizopo jengo la kufulia zianze kutumika.

Dkt. Mfaume ametoa maelekezo hayo akiwa ameambatana na timu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI mkoani Katavi kwaajili kukagua miradi ya Afya na kufuatilia ufanisi na utendaji wa watoa huduma za Afya na wamebaini vifaa vilivyoletwa katika hospitali hiyo ikiwemo mashine ya kufulia nguo na kukausha pamoja na pasi vimekaa zaidi ya mwaka mmoja bila kutumika.

“Mashine hii ya kufulia imepokelewa zaidi ya mwaka mmoja lakini kunamashine ya kukaushia nguo tumeiona na ‘stand by generator’ lakini watumishi wa hapa kwa taarifa tulizonazo wanafua kwa kutumia mikono.

Tumeona mabeseni hapa wakati mama Samia alikuwa na nia ya dhati ya kuwasaidia watendaji na ukiangalia thamani ya vifaa ni kubwa mno kuvileta na kuviweka kwenye eneo kama hili haipendezi na wala haifurahishi na Rais Samia hafurahishwi na jambo kama hili na kila kiongozi hatofurahishwa na kitu kama hiki” amesema Dkt. Rashid Mfaume

Natoa mwezi mmoja mashine hizi zianze kutumika mara moja’ amesema Dkt. Mfaume.

About the author

mzalendo