Featured Michezo

HAZINA SPORTS CLUB YAREJEA NA KOMBE LA UBINGWA WA MASHINDANO YA SHIMIWI

Written by mzalendoeditor

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, akipokea kombe la ubingwa wa mashindano ya SHIMIWI kwa upande wa mpira wa miguu kutoka kwa Kapteni wa timu ya mpira wa Miguu kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Asegelile Mboya (kulia) yaliyofanyika katika viwanja vya Samora na Chuo cha Mkwawa Mkoani Iringa kuanzia Septemba 27 hadi Oktoba 14, 2023.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, akipokea kombe la Mshindi wa tatu wa mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kwa upande wa mpira wa pete kutoka kwa Kapteni wa timu ya mpira wa pete wa Wizara ya Fedha, Bi. Halima Juma (kulia) yaliyofanyika katika viwanja vya Samora na Chuo cha Mkwawa Mkoani Iringa kuanzia Septemba 27 hadi Oktoba 14, 2023.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Hazina Sports Club baada ya kumkabidhi Naibu Katibu Mkuu huyo kombe la mshindi wa kwanza kwa mpira wa miguu na mshindi wa tatu kwa mpira wa pete walilopata kwenye mashindano ya SHIMIWI yaliyofanyika katika viwanja vya Samora na Chuo cha Mkwawa Mkoani Iringa kuanzia Septemba 27 hadi Oktoba 14.

Picha ya kombe la ubingwa wa mpira wa miguu na kombe la mshindi wa tatu kwa mpira wa pete ambayo Hazina Sports Club iliyapata katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yaliyofanyika katika viwanja vya Samora na Chuo cha Mkwawa Mkoani Iringa kuanzia Septemba 27 hadi Oktoba 14 yaliyokutanisha Wizara zote.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)

About the author

mzalendoeditor