Featured Kimataifa

ZIARA YA KITAIFA YA RAIS SAMIA AANDALIWA DHIFA YA KITAIFA IKULU YA INDIA (RASHTRAPATI BHAWAN)

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa India Mhe. Droupadi Murmu mara baada ya kuwasili Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) New Delhi kwa ajili ya kushiriki Dhifa ya Kitaifa nchini humo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa India Mhe. Droupadi Murmu wakati wa Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa mara baada ya kuwasili Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) New Delhi kwa ajili ya kushiriki Dhifa ya Kitaifa nchini humo

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa India Mhe. Droupadi Murmu kabla ya kushiriki Dhifa ya Kitaifa katika Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) iliyopo New Delhi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Serikali ya India mara baada ya kuwasili Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) New Delhi kwa ajili ya kushiriki Dhifa ya Kitaifa nchini humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais wa India Mhe. Jagdeep Dhankhar katika Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) New Delhi kabla ya kushiriki Dhifa ya Kitaifa nchini humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili Ikulu ya India (Rashtrapati Bhawan) New Delhi kwa ajili ya kushiriki Dhifa ya Kitaifa nchini humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa na Rais wa India Mhe. Droupadi Murmu katika Ikulu ya India.

About the author

mzalendoeditor