Featured Kitaifa

CHONGOLO ATETA NA BALOZI WA CHINA JIJINI DAR ES SALAAM

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Godfrey Chongolo, Septemba 29, 2023, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Bi Chen Mingjian, aliyeambatana na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, jijini Dar Es Salaam, yaliyolenga kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji kati ya pande hizo mbili, pamoja na kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidugu baina ya nchi za Tanzania na China chini ya uongozi wa Vyama vya CCM na CPC, mtawalia.

About the author

mzalendoeditor