Featured Michezo

YANGA YAJIWEKA NJIA PANDA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Yanga imejiweka njia panda kutinga hatua ya makundi ya Michuano ya Klabu bingwa Afrika baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wageni Al Hilal kutoka nchini Sudan mchezo uliomalizika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Yanga walipata bao kupitia Mshambuliaji wao hatari  Fiston Mayele dakika ya 50 huku n Al Hilal wakipata bao dakika ya 67 likifungwa na  Mohamed Youseif aliyetokea benchi.

Kwa matokeo hayo Yanga wamejiweka katika nafasi finyu huku  wakihitaji kwenda kushinda au kutoka sare ya kuanzia mabao 2 mchezo utakaopigwa mwishoni mwa wiki nchini Sudan.

Kama Yanga wataweza kutolewa wataangukia katika mtoani wa kombe la Shirikisho Afrika.

About the author

mzalendoeditor