Featured Kitaifa

MILIMA YA TAO LA MASHARIKI (EAMCEF) LAZIMA IHIFADHIWE-HOSEA

Written by mzalendoeditor
Na.Farida Mangube-Morogoro.
Afisa msaidizi kitengo cha tathimini na ufatiliaji wa miradi kutoka mfuko wa hifadhi ya milima ya tao la Mashariki (EAMCEF) Steve Hosea amesema milima ya tao la mashariki ni lazima ihifadhiwe hasa na wananchi wanaoishi katika milima hiyo kwani imekuwa ikiwaongezeaa kipato kupitia shughuli mbalimbali kama ufugaji Ng’ombe na mbuzi wa maziwa pamojaa na ufugaji nyuki.
Amesema hayo wakati wa mkutano wa wadau wa kuboresha rasimu ya mkakati wa utalii wa mazingira wa hifadhi za misitu asilia na hifadhi ya taifa katika milima ya tao la mashariki unaoendelea mjini Morogoro
Hosea amesema lengo la EAMCEF ni kuhakikisha milima ya tao la mashariki inahifadhiwa na jamii inayoizunguk na ndio maanaa imekuwa ikiwezesha shughuli mbalimbali kama ya kuwaongezea kipato kwa kuanzisha miradi ya ufugaji kuku,na masuala ya tafiti katika milima kupitia taasisi mbalimbali zinazofanya utafiti kama Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania(TAFORI).
“Tumekuwa tukitoa fedha kwenda moja kwa moja kwenye hifadhi ya misiti asili kwa ajili ya masuala ya usimamizi na kuwezesha shughuli za utalii ikolojia, sisi ni wadau wakubwa na wa muhimu katika kutunza na kuhifadhi milima ya tao la mashariki ndo maana tukaona tufanye hayo ili kuhakikisha tunapata ongezeko la utalii nchini,”amesema.
Aidha amesema watalii wengi kwa sasa wameona hakuna jipya sasa kwenye kuangalia wanyama wengi wao wameonekana kuja nchini kuangalia ualisia wa mazingira hivyo wameonelea kuwezesha shughuli kwenye hayo mazingira kwa kutoa fedha kwa ajili ya kusafisha njia za watalii wanapopita kwenda kuangalia miti asili.
“Wengine wanakuja kw ajili ya kupata hewa saafi, kuangalia ndege mbalimbaa na viumbe ambavyo vimerkuwa havipatikaani mahala popote duniani kama vinyonga wa pembe tatu wanaopatikana Amani, na hiyo ni moja ya kazi inayofanyika kwenye hifadhi,”amesema
Naye Kaimu mkurugnzi mkuu wa TAFORI Allan Kazimoto akifungua mkutano huo amesema watafiti kutoka Tafori walifanya tafiti kwenye hifadhi nane(8) za misitu asilia na hifadhi moja ya taifa na kuona changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa kuboreshwa kutokana na tathimini iliyofanyika.
Kazimoto amesema changamoyto ya miundombinu kaamaa barabara ambayo hasa kipindi cha mvua kusababisha kutopitika na nkupelekea wageniwachache na wa msimu ambapo ushirriki wa jamii ni wastani wa asilimia 18.56 tu na kwamba hiyo usababishwa na vijiji vichache kuwa vyanzo vya vivutio.
Aidha alieleza kuwa tathimini nyingine ni ushiriki wa wananchi kwenye uhifadhi endelevu wa misitu ambapo ilionyesha kuwa na zaidi ya asilimia 98 katika hifadhi zote wanashiriki ipasavyo na kuwa hiyo ni kutokana na wanaelimu ya kutosha juu uhifadhi nan kutambua umuhimu wa uwepo wa milima.
“Tathimini zote hizo na nyingine zinaonyesha wananchi wanatambua uwepo wa utalii wa mazingira ila ushiriki wao ni mdogo unaosababishwa na changamoto mbalimbali za ukosefu w miundombinu bora na ufinyu wa elimu ya utalii wa mazingira asilia,upungufu wa masoko,”amesema.
Afisa taarifa wa Tafori na mtafiti Jofrey Njovangwa amesema utafiti uliofanyika ulikuwa kuangalia mchango wa utalii wa mazingira au wa ikolojia kwenye uhifadhi wa milima ya tao la mashariki na hifadhi zilizotumika kwenye utafiti ni pmoja na Amani, Chome, Nilo, Mgamba, Mkingu, Uluguru, Udzungwa, Uzungwa na Kilombero.

About the author

mzalendoeditor