Featured Kitaifa

KAMISHNA WA MADINI ATEMBELEA MGODI WA BULYANHULU

Written by mzalendoeditor

Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahman Mwanga ametembelea Mgodi wa Bulyanhulu uliopo wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga katika ziara iliyolenga kufuatilia shughuli za uzalishaji.

Vile vile Dkt. Mwanga ametembelea maeneo ya machimbo chini ya ardhi (underground) na mitambo ya uchenjuaji (process plant).

Ziara hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kufuatilia shughuli za uzalishaji pamoja na changamoto zinazoikabili Mgodi wa Bulyanhulu na kujua mwenendo wa uzalishaji kwa sasa.

Kamishna alizungumza na uongozi wa mgodi na kusisitiza kuwa wawe karibu na Wizara ya Madini pamoja na taasisi zake pindi wanapopata changamoto yoyote na wasisite kutoa taarifa.

Pia alisisitiza pindi mgodi unapotaka kufanya manunuzi au kubadilisha mtambo wowote ni vema wakatoa taarifa Tume ya Madini kwa hatua stahiki .

Halikadhalika aliutaka uongozi wa mgodi kufikiria njia bora ya kuhakikisha madini yote yanayozalishwa mgodini yanaongezewa thamani hapa nchini.

Naye, Meneja Mkuu wa Mgodi Cheick Sangare alieleza kuwa mgodi huo upo tayari kushirikiana na Serikali.

About the author

mzalendoeditor