Featured Kitaifa

CCM YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA BANDARI YA TANGA

Written by mzalendoeditor

Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Musa Msabimana kushoto akiwaonyesha
maboresho yaliyofanywa na Serikali bandarini hapo wakati wa ziara ya
Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Tanga iliyotembelea Bandari hiyo kwa
ajili ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika mradi wa kimkakati
wa maboresho kushoto Mwenye shati la kijani ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu kushoto akiwa na Mbunge wa Jimbo la
Mkinga (CCM) na Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Tanga Dastan Kitandula
wakitembelea Flow Meters za Bandari
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM mkoa wa Tanga wakionyeshwa namna Floor Meter zinavyofanya kazi
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni MNEC wa Mkoa wa Tanga Ratco
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Musa Msabimana akizungumza kuhusu maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye Bandari ya Tanga
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Musa Msabimana akizungumza kuhusu maboresho makubwa yaliyofanywa kwenye Bandari ya Tanga
MNEC wa Mkoa wa Tanga Ratco akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tanga Dkt Aisha Kigoda akieleza jambo wakati wa ziara hiyo
MWENYEKITI wa UVCCM Mkoa wa Tanga Rasul Shandala akizungumza wakati wa ziara hiyo

MBUNGE
wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Wabunge wa Mkoa wa Tanga akizungumza wakati wa ziara hiyo

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge akichangia jambo wakati wa ziara hiyo

Na Oscar Assenga,Tanga.

CHAMA
cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimempongeza Rais Samia Suluhu na
Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa katika
Bandari ya Tanga ambao utawezesha kuijengea uwezo wa ufanisi.

Pongezi
hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Dkt Henry Shekifu
wakati wa ziara ya kamati ya Siasa ya Mkoa wa Tanga ilipotembelea
Bandari ya Tanga kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika
mradi wa kimkakati wa maboresho ya Bandari hiyo.

Akizungumza
mara baada ya kutembelea bandari hiyo Dkt Shekifu alisema katika kipindi
kifupi cha miaka mitano hali imekuwa tofauti na miaka ya nyuma huku
akieleza eneo ambalo wametembelea ni hapo walipo wapo kwenye gati ambalo
kwenda chini ni mita 13 .

Alisema kwa sasa eneo la karibia mita
200 zimejengwa kutoka ukuta wa zamani kuja ndani ili kuweza kuruhusu
meli kubwa ziingie ambapo zimetumika fedha fedha nyingi sana na zitakuwa
na tija kutokana na Bandari kuwa lengo la Biashara.

Mwenyekiti
huyo alisema faida ambayo ni kubwa itawezesha meli kubwa kuingia Tanga
na zikiingia uchumi wa Tanga utapanuka na hivyo kuchochea maendeleo kwa
mkoa wa Tanga na wananchi wake.

“Kwa kweli hapa kumefanyika kazi
kubwa sana na tumsifu Rais Samia Suluhu,Serikali imefanya kazi nzuri na
watendaji sisi kama chama tunaona wamewatenda haki na wamekuwa
waaminifu katika kutekeleza wajibu wao”Alisema Mwenyekiti huyo wa CCM
Mkoa.

Alisema kwa sababu ukizungumzia Bandari unazungumzia
uchumi mkoa wa Tanga sasa hapo itakuwa ni jicho na itafungua uchumi wa
mkoa wa Tanga hatua ambayo itachochea kasi ya maendeleo na hivyo
kuwainua kiuchumi.

Aidha alisema anaamini CCM wana kila sababu
ya ya kusema wana uwezo wa kuongoza nchi na watahakikisha wanafanya kazi
ya kutekeleza yake ambayo wanahaidi wananchi.

Hata hivyo
alisema upanuzi huo na wingi wa mizigo itakayotoka hapo haitakuwa na
mahali ya kuwekwa sasa wanaiomba serikali suala la kurekebisha barabara
za kutoka Tanga Bandari kwenda nje ni muhimu sana na kuna bandari ambapo
zitawekwa kontena Mwambani sasa zitakuwa ni nyingi kuzitoa nje ya mkoa
sasa kama hauna barabara ya kuzitoa maana yake utachelewa kuwafikia wa
wateja.

“Sasa hapa ndio kutakuwa ni Jicho mizigo itatoka hapa
itapelekwa nchi nyengine zitaletwa hapa na kupakizwa kwenye treni na
kupelekwa nchi nyengine na hivyo kuinua uchumi wa mkoa wa Tanga”Alisema

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwakilishi wa
Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge alisema
suala la reli na Bandari ni jambo la Msingi kuhakikisha wanapata
shehena za kutosha kwenye Bandari ya Tanga.

Alisema wanamshukuru
Rais kwa fedha nyingi alizotoa bilioni 429.1 ambapo awamu ya kwanza
ilikuwa ni Bilioni 172.3 na awamu ya pili Bilioni 256.8 ambazo
zimewezesha maboresho makubwa kwenye Bandari hiyo ikiwemo ununuzi wa
mitambo.

Mbunge Ulenge alisema lakini pamoja na hayo bila
mikakati ya kuongeza shehena ina maana bandari hiyo bado itakuwa
haifanyi vziru hivyo wanaomba Reli ya Tanga hadi Arusha ifanye kazi na
hiyo imeshakarabiwa karibia kilomita 400 lakini mpaka sasa haijafanya
kazi.

“Tunaiomba Serikali ihakikishe Reli ya Arusha hadi Tanga
iweze kufanya kazi ili tupate shehena kutoka Arusha na Kilimanjaro
ambao wanakimbilia Bandari ya Mombasa Kenya wakati kuna bandari ya
Tanga”Alisema

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Kaimu
Meneja wa Bandari ya Tanga Musa Msabimana alisema ili Bandari iweze
kufanya kazi kwa ufanisi lazima uinganishwe na reli kwa sababu bandari
mzigo unapokuja haiishii bandarini lazima uenda kwa wananchi.

Alisema
kwamba njia rahisi ambayo sio ya gharama kubwa ni reli sasa kuna
kipande cha reli kinachounganisha Bandari ya Tanga na reli kipo
hakifanyi kazi sasa wao TPA wameamua kufanyia kazi ili kuweza kikifufua.

“Hii sio mara ya kwanza kama mnakumbuka hata bandari ya Mwanza
waliwahi kutengeneza meli wakiamini kwamba Bandari ya Mwanza meli
ikifanyia kazi Bandari itafanya kazi lakini pia nakumbuka miaka sita
iliyopita waliwahi kununua injini za reli kwa ajili ya kuwezesha kutoa
mizigo bandarini kuunganisha na reli hivyo tutalifanyia kazi hilo kwa
muda mfupi mzigo utakaotioka uende kwa njia ya reli”Alisema

About the author

mzalendoeditor