Featured Kitaifa

JENGO LA KITEGA UCHUMI LA GHOROFA TANO LA SUMA JKT LAZINDULIWA JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Venance Mabeyo,akimsikiliza Mkurugenzi wa SUMA JKT Kanali Petro Ngata,kabla ya kuzindua jengo la Kitega Uchumi la ghorofa tano lililojengwa na Shirika la Uzalishajimali(SUMAJKT) lijulikanalo Kama SUMAJKT house lililogharimu shilingi Bilion 2.8 hadi kukamilika kwake lililopo Medeli East Jijini Dodoma.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Venance Mabeyo,akizindua jengo la Kitega Uchumi la ghorofa tano lililojengwa na Shirika la Uzalishajimali(SUMAJKT) lijulikanalo Kama SUMAJKT house lililogharimu shilingi Bilion 2.8 hadi kukamilika kwake lililopo Medeli East Jijini Dodoma.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Venance Mabeyo,akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua jengo la Kitega Uchumi la ghorofa tano lililojengwa na Shirika la Uzalishajimali(SUMAJKT) lijulikanalo Kama SUMAJKT house lililogharimu shilingi Bilion 2.8 hadi kukamilika kwake lililopo Medeli East Jijini Dodoma.

Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele,akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Kitega Uchumi la ghorofa tano lililojengwa na Shirika la Uzalishajimali(SUMAJKT) lijulikanalo Kama SUMAJKT house lililogharimu shilingi Bilion 2.8 hadi kukamilika kwake lililopo Medeli East Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa SUMA JKT Kanali Petro Ngata,akielezea mikakati itakayotumika katika jengo la Kitega Uchumi la ghorofa tano lililojengwa na Shirika la Uzalishajimali(SUMAJKT) lijulikanalo Kama SUMAJKT house lililogharimu shilingi Bilion 2.8 hadi kukamilika kwake lililopo Medeli East Jijini Dodoma.

MUONEKANO wa jengo la Kitega Uchumi la ghorofa tano lililojengwa na Shirika la Uzalishajimali(SUMAJKT) lijulikanalo Kama SUMAJKT house lililogharimu shilingi Bilion 2.8 hadi kukamilika kwake lililopo Medeli East Jijini Dodoma.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Venance Mabeyo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua jengo la Kitega Uchumi la ghorofa tano lililojengwa na Shirika la Uzalishajimali(SUMAJKT) lijulikanalo Kama SUMAJKT house lililogharimu shilingi Bilion 2.8 hadi kukamilika kwake lililopo Medeli East Jijini Dodoma.

……………………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Venance  Mabeyo amewataka Maafisa na Askari wa JKT kuendelea kubuni miradi mbalimbali ya uzalishajimali kwa lengo la kuchangia ukuaji wa maendeleo ya Taifa letu.

Jenerali Mabeyo ameyasema leo Juni 28,2022  wakati akizindua jengo la Kitega Uchumi la ghorofa tano lililojengwa na Shirika la Uzalishajimali(SUMAJKT) lijulikanalo Kama SUMAJKT house lililogharimu shilingi Bilion 2.8 hadi kukamilika kwake lililopo Medeli East Jijini Dodoma.

Jenerali Mabeyo amesema amevutiwa na utaratibu wa Kuchukua Fedha ambayo JKT inapata katika kazi zake na kuwekeza katika miradi na kuwataka kuendelea kubuni zaidi miradi ambayo itawanufaisha zaidi ili jeshi liendelee kujiimarisha na kutekeleza miradi kwa uaminifu.

“Na nina imani kuwa  mnaendelea kujijengea imani na uzoefu mbalimbali wa kutekeleza miradi ambayo ni ya kwenu, watu binafsi au taasisi binafsi hapo baadaye, ninawapongeza sana kwa kujitambua kujiamini na kujithamini ninyi wenyewe,” amesema jenerali Mabeyo.

Amezipongeza mamlaka mbalimbali za serikali ikiwemo halmashauri ya jiji kwa kuwapa ushirikiano wa kupata vibali vya ujenzi bila vikwazo, na kutoa shukrani za dhati kwa kushirikiana na jeshi kwa jeshi katika kulijenga taifa, na kuwahakikishia kwamba jeshi litaendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi hizo na waendelea kutoa ushirikiano.

Jenerali Mabeyo, amesema  jengo hilo la SUMAJKT house litatumika katika shughuli mbalimbali za kupangisha ikiwemo huduma za kibenki ofisi na kwa kuwa jijiji la Dodoma linakuwa kwa kasi  amewapongeza kwa kuwasaidia wadau mbalimbali kupata nafasi kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.

 “Niwatake mlitunze jengo hilo kama kumbukumbu ya utumishi na jasho lenu, mkilitunza vizuri litadumu kwa muda mrefu na kuendelea kuvutia katika jiji letu, niwakumbushe methali ya kiswali kitunze kidumu,” amesema.

Katika hatua nyingine amewataka Maafisa na Askari wanaomaliza muda wa Utumishi Jeshini wasiache kutoa mawazo mazuri ndani ya Jeshi kubuni miradi ya maendeleo hata Kama muda wao wa Utumishi Jeshini unafika kikomo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema SUMA JKT itaendelea kubuni miradi mingine mikubwa kwenye sekta mbalimbali ili kuwezesha Shirika kuongeza uwezo kama dira na dhima ya Shirika zinavyoelekeza kutimiza malengo ya kuchangia uendeshaji wa shughuli za JKT na kujenga uchumi wa Taifa.

“Nawapongeza wakuu wa mradi makampuni na Kada zote za ujenzi wa SUMA JKT ambao wameweza kutoa gawio na kuwezesha ujenzi wa jengo hilo, ujenzi wa jengo hilo umejengwa na SUMA JKT,” amesema Brigedia Jenerali Mabele.

Katika hatua nyingine  Meja Jenerali Rajabu Mabele amemshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance  Mabeyo kwa kuzindua Jengo hilo na kuahidi kuyazingatia yale yote ambayo Mkuu huyo wa Majeshi amewaambia.

Awali Mkurugenzi wa SUMA JKT Kanali Petro Ngata,amesema, jengo hilo la kitega uchumi cha Shirika la uzalishaji Mali la SUMA JKT, la Jeshi la Kujenga Taifa ni la ghorofa Tano zenye ‘floor’ zilizo wazi ikiwa ni mahususi kwa ajili ya kupangishwa kibiashara.

Amesema hadi kukamilika kwa ujenzi huo jumla ya Sh. Bilioni 2.8 zimetumika, na kwamba usanifu wa jengo hilo umehusisha matumizi mbalimbali ikiwemo eneo la ground floor limesanifiwa kwaajili ya taasisi za kifedha ambalo linakidhi kwa mahitaji ya biashara za kifedha.

“Ghorofa ya Kwanza hadi ya Nne zimesanifiwa kwa ajili ya shughuli za ofisi, ghorofa ya Tano imesanifiwa Kwaajili ya ofisi ya meneja wa jengo, eneo la nje limesanifiwa Kwa ajili ya maegesho ya magari,” amesema Kanali Ngata.

About the author

mzalendoeditor